Dkt. Bashiru: Siyo kweli kwamba CCM itatumia wingi wao Bungeni kubadilisha Katiba ili kumuongezea muda Rais Magufuli kukaa madarakani!

Bwasheee Kukosa Mbowe CDM ingekuwa ishakufa!! CDM imesimama kwa Juhudi za Mwamba MBOWE!! Fedha za ruzuku haziwezi kujenga Makao Makuu kwa sasa ,Subiri CDM ichukue nchi ndio ijenge HQ.
Hahahaaaa....... Ngoja tusubiri.

Sitaki nionekane Kibwengo by Benard Membe!
 
Ally Kessy aliyeanzisha hiyo hoja bungeni ni mpinzani, Job ndugai aliyemuahidi kessy kuwa ahifadhi hoja yake hadi bunge hili (bahati mbaya hakufanikiwa kurudi) ili ifanyiwe kazi na kumhakikishia kuwa itapitishwa kwa nguvu na kumlazimisha jiwe kuongeza muda naye ni mpinzani. Tatizo la vijana wa ccm mna usahaulifu mkubwa
Ya ni kweli hata mwenyekiti wetu wa CCM mh Mbowe alibadili katiba ya chama chetu cha CCM ili aendelee kututawala milele kwa madai kwamba hajaona mtu sahihi wa kumuachia kiti cha uongozi. Pia inaonekana hata siku chama chetu kikishika madaraka atakuwa wa kwanza kubadilisha katiba ya ukomo wa madaraka ili aweze kuendelea kututawala milele kama alivyofanya ktk katiba ya chama chetu. Ikiwa alibadilisha katiba ya chama kwa kigezo cha kukosa mtu sahihi wa kuongoza chama chetu je kwa upande wa nchi itakuaje? Ebu tumia akili uliyopewa na muumba wako kujiongeza na sio kutumia akili uliyochomekewa na viongozi wa kisiasa ambao bila shaka wanaangalia masilahi ya matumbo yao na sio matumbo ya wanachama wao au wananchi wao
 
Sisi watanzania 84% tunataka katiba ibadilishwe ili huyu Rais mwema mwenye Moyo wa huruma na upendo kwa RAIA wake atawale milele na lazima tutaandamana nchi nzima kushinikiza hilo jambo
Hatuwezi kukubali kukosa Rais kama Magufuli ila wapiga dili lazima muumie maana mianya imeziba kabisa
 
Speaker mmeshaongea naye kwamba aachane na hiyo hoja huko Bungeni?
Kwa kauli hii ya Katibu mkuu huo sasa ni msimamo wa Chama.

I believe jambo hili sasa limefikia mwisho.
 
Huyu nae eti alikua anafundisha wanafunzi wa chuo, khaaaaaah aibu naona mie.
 
Katibu mkuu wa CCM, Dkt. Bashiru amekanusha uvumi unaoenezwa na wapinzani kwamba wabunge wa CCM watatumia wingi wao bungeni ili kumuongezea Rais Magufuli muda wa kukaa madarakani iwe zaidi ya miaka 10.

Dkt. Bashiru amesema Rais Magufuli atahudumu madarakani kwa miaka 10 kwa mujibu wa katiba ya sasa na kwamba propaganda za wapinzani hasa Chadema zipuuzwe.

Nawatakia ninyi nyote Dominica yenye baraka!

Maendeleo hayana vyama!
Mmm... This smells fishy; isije ikawa ni tahadhari toka ndani ya CCM inatumwa kimkakati kwa JPM kupitia mgongo wa "wapinzani" kwamba asifikirie kabisa kuanzisha mchakato wa kujiongezea muda. Ni "wapinzani" gani hao ambao bado wanasikika kwa nguvu hadi kwa KM wa CCM? Eti uvumi. Huyu ameanza kujibizana na kivuli chake mwenyewe.

Anyway, nadhani sasa Bashiru na mashabiki uchwara wa CCM wataanza kuelewa maana halisi ya upinzani na wapinzani - watakapoanza kushuhudia wakipishana na vivuli vyao njiani!
 
Kwa kauli hii ya Katibu mkuu huo sasa ni msimamo wa Chama.

I believe jambo hili sasa limefikia mwisho.
Basi itakua imekaa vizuri, maana Kessy na Ndugai waliliweka vibaya ingawa nia yao ilikua ni "kujipendekeza" kwa Mwenyekiti, ukichukulia wakati ule tulikua tunaelekea kwenye kura za maoni.

Katibu mkuu alitakiwa aliongee katika mtizamo huo ndani ya chama chake kuliko kuliweka kama vile ni la vyama vya upinzani.
 
Sisi watanzania 84% tunataka katiba ibadilishwe ili huyu Rais mwema mwenye Moyo wa huruma na upendo kwa RAIA wake atawale milele na lazima tutaandamana nchi nzima kushinikiza hilo jambo
Hatuwezi kukubali kukosa Rais kama Magufuli ila wapiga dili lazima muumie maana mianya imeziba kabisa
Kuna wapiga dili zaidi ya hao wakurugenzi ambao ni makada wa ccm na waliowasaidia kushinda uchaguzi na sasa mnawatumbua kwa wizi wa pesa za wananchi katika manunuzi na katika miradi?
 
Ya ni kweli hata mwenyekiti wetu wa CCM mh Mbowe alibadili katiba ya chama chetu cha CCM ili aendelee kututawala milele kwa madai kwamba hajaona mtu sahihi wa kumuachia kiti cha uongozi. Pia inaonekana hata siku chama chetu kikishika madaraka atakuwa wa kwanza kubadilisha katiba ya ukomo wa madaraka ili aweze kuendelea kututawala milele kama alivyofanya ktk katiba ya chama chetu. Ikiwa alibadilisha katiba ya chama kwa kigezo cha kukosa mtu sahihi wa kuongoza chama chetu je kwa upande wa nchi itakuaje? Ebu tumia akili uliyopewa na muumba wako kujiongeza na sio kutumia akili uliyochomekewa na viongozi wa kisiasa ambao bila shaka wanaangalia masilahi ya matumbo yao na sio matumbo ya wanachama wao au wananchi wao
anzisha post ya mbowe, hapa tunaongelea kuhusu jiwe na kuongezewa muda wa kukaa madarakani kama rais. Mbowe hajawahi kuwa rais wa nchi.
 
Kuna wapiga dili zaidi ya hao wakurugenzi ambao ni makada wa ccm na waliowasaidia kushinda uchaguzi na sasa mnawatumbua kwa wizi wa pesa za wananchi katika manunuzi na katika miradi?
Hii ni serikali makini sana
Hata akiwa waziri akifanya ubadhirifu lazima awajibishwe
Zamani watu walikua wanalindana lakini sio awamu hii ya Rais mwema mwenye Moyo wa huruma na upendo kwa RAIA wake
 
kila siku mnatuimbia kuwa nidhamu imerudi toka awamu ya tano ilipoingia madarakani, ajabu ni kuwa kila siku mnatumbuana tena viongozi sasa hao wabadhirifu wanatoka awamu gani? Mkiwa waongo msiwe wasahaulifu
 
Yaani mkuu kwa kawaida waovu sio rahisi kuwamaliza kabisa Ndio maana unaona tunawatumbua na Tunajua bado wapo ila ni wachache mnoo
 
ndio maana nikakwambia mkiwa waongo msiwe wasahaulifu maana kila siku mnaimba kuwa magufuli kafuta wazembe na wabadhirifu, kaleta nidhamu ya kazi lakini ajabu ni kuwa utumbuaji ndio unaongezeka kila siku
 
Saccos ya wachaga ime disintegrate hadi mwisho, sasa hawana hoja, kazi yao kusema Mh. Rais anataka kuongeza muda kwa kubadili katiba.
 
ndio maana nikakwambia mkiwa waongo msiwe wasahaulifu maana kila siku mnaimba kuwa magufuli kafuta wazembe na wabadhirifu, kaleta nidhamu ya kazi lakini ajabu ni kuwa utumbuaji ndio unaongezeka kila siku
Awamu hii inawajibisha na itaendelea kuwajibisha viongozi waovu tofauti na zamani watu walikua wanalindana
 
Hujajibu swali, hao viongozi wabovu wametoka wapi wakati kwa miaka mitano mmekuwa mkijinasibu kuwa jiwe limemaliza viongozi wabadhirifu na watumishi waovu na wazembe, na pia mmekuwa mkijinasibu kuwa jiwe anachagua viongozi bora haijawahi kutokea? Maana wengi wa wanaotumbuliwa sasa hivi ni wateule wa jiwe?
 
Ndiye aliyesema CCM haitotumia Wasanii kwenye Kampeni.

Tumsamehe bure maana nadhani mengine naye humkuta tu kama suprise kama sisi wa huku nje.
 
Back
Top Bottom