Dkt. Bashiru: Unaposhukuru na kusifia unapopewa haki yako unakuwa hauna "maana"

Dkt. Bashiru: Unaposhukuru na kusifia unapopewa haki yako unakuwa hauna "maana"

Hii kauli ya Dr Bashiru kwa MVIWATA nataka niiangalie kikatiba na kiBiblia zaidi

Sitajali hata kama yeye alikuwa akishukuriwa na Kusifiwa wakati anatimiza Majukumu yake ambayo kwayo alilipwa mshahara

"Ukishukuru na Kusifu unapopewa Haki yako unakuwa hauna maana"

Wabunge husemaga: Mh Spika nakushukuru kwa kunipa nafasi ya kuchangia

Sasa utajiuliza Mbunge kuchangia Hoja ni Haki ya Msingi au Hisani ya Spika?

Itaendelea...
CCM imejaa majitu majinga sn hayajui tofauti ya haki na hisani kazi kubwa ni kusifia na kushukuru
 
Labda ashukuriwe na sukuma gang. Yeye ni Sehemu ya hii tabia chafu ya kumsifia rais hata kwa mambo ambayo hapaswi kushukuriwa.
Eti bashiru leo anakemea watu kumshukuru rais!

Hii nchi unafki na uchumia tumbo unaiangamiza sana.
 
Awamu iliyopita ndio waanzilishi wa hizi sifa zilizotamalaki nchini! Hatukuwahi kumuona akikemea alipokuwa kwenye chungu cha asali
Awamu iliyopita alikuwa anapenda kusifiwa kwa alichokifanya na kikiwa hadharani ila hii kama ni baya lisilokuhusu binafsi lazima usifie
 
Kusema mh spika nashukuru kwa kunipa nafasi ni heshima ya kiti Tu, haina maana hata kama hatosema hivyo, ni Sawa na mtu akikikuuliza nikuongezee maji? Ukamjimbu No thank you, ungeweza kusema No Tu ikatosha

But Rais kulete maji kwenye mkoa ni moja ya majukumu yake ndio maana akawa kiongozi wetu na analipwa Kwa kuwa kiongozi wetu na ana ulinzi wa kutosha Kwa kazi hiyo sasa why tumshukuru?
Naona watanzania mnaanza kuona mwanga; kama ni kushukuru,basi ni walipa Kodi zao kwa uaminifu na kila mtanzania anayetoa huduma au kazi kwa ajili ya Taifa letu,Muda wa kumshukuru ni pale atapostaafu kwa amani na uongozi uliotukuka sio akipokea ndege ambazo zimelipwa kwa kodi
 
Ngoja nifuatilie kama Bashiru hushukuru anapochangia.

Lakini mimi ni sapota wa Bashiru kuwa hakuna kumsifia Hangaya huku tuko gizani, maji hakuna na rushwa kubwa kubwa zikirindima, eti ni kula kwa urefu wa kamba.
Mheshimiwa Spika niende moja kwa moja kwenye hoja yangu ya msingi
 
Hii kauli ya Dr Bashiru kwa MVIWATA nataka niiangalie kikatiba na kiBiblia zaidi

Sitajali hata kama yeye alikuwa akishukuriwa na Kusifiwa wakati anatimiza Majukumu yake ambayo kwayo alilipwa mshahara

"Ukishukuru na Kusifu unapopewa Haki yako unakuwa hauna maana"

Wabunge husemaga: Mh Spika nakushukuru kwa kunipa nafasi ya kuchangia

Sasa utajiuliza Mbunge kuchangia Hoja ni Haki ya Msingi au Hisani ya Spika?

Itaendelea...
hoja hii ina mashiko sana, Dr Bushiru umepiga penyewe !!
 
Hata watoto wanapopikiwa chakula na mama yao humshukuru baada ya kula!!
Husema "Mama asante kwa chakula"
 
Awamu iliyopita alikuwa anapenda kusifiwa kwa alichokifanya na kikiwa hadharani ila hii kama ni baya lisilokuhusu binafsi lazima usifie
Uzuri au ubaya wa jambo ni subjective! Wewe unayeona watu kufilisiwa au bureau de change kuvamiwa ni sawa vivyo hivyo kuna watu wanaona ni sawa vyeti feki kulipwa mafao yao. Kiufupi kuimba ni kupokezana
 
Back
Top Bottom