Dkt Bashiru: Waliotaka kutuchonganisha wameshindwa na kulegea

Dkt Bashiru: Waliotaka kutuchonganisha wameshindwa na kulegea

Mfa maji haishi kutapatapa.
Leo hii huyu Ni Kama mzee Halima tu.
Alinyanyasa sana watu na kutuletea wsgombea wasio na sifa za kua wabunge halafu alipoingia ikulu ndio alitegemea kuabudiwa Kama mwendazake lkn mipango haikua na Majaliwa.
Sasa hivi yeye na mzee Halima level moja
Watanzania wanamwamini akigombea anashinda tu
 
Nani aliyetaka kumuhujumu Mama Samia asirithi kiti baada ya mwendazake kukata umeme? Nyie ndio mliotaka kuwachonganisha wananchi!
 
Bashiru ana maadui wengi sana ndani ya chama , hasa kukata mizizi ya wizi ndani ya mikoa na ngazi ya wilaya. Lakini ameonyesha bado ni shupavu na ujengaji wake wa hoja za mantiki ni hazina kubwa aliyonayo. Hata kama kuna mapungufu yalitokea baada ya JPM, bado ninaamini mama atamlinda na amor ubalozi nchi yoyote baada ya miaka hii minne ya ubunge. Kama yeye ni mlangila nina imani hawezi gombea ubunge wa jimbo. Ref, watoto wa Nyerere hamna anayepata ubunge Musoma sababu wazanaki ni minority Musoma , Na kule Bukoba hali kadhalika Mlangila hawezi kupata ubunge licha ya kwamba ni watawala kabla ya uhuru. Kwa intelect yake na uzalendo wake Bashiru atakuwa Balozi huko mbeleni na hasa kwenye utawala wa mama Samia hawezi kumtupa kijana kipenzi wa JPM jamii ya wastaarabu haruwezi kumwelewa na usemi wakazi iendelee ni pamoja na kuenzi mema ya marehemu. Bashiru ndiye kafanya chama kijitegemee kifedha baada ya kuhamishia mapato yote makao makuu. HONGERA Bashiru taifa limefiwa ,lakini mwenzetu meguswa zaidi na kifo cha marehemu , muzilankende mwenzake na JPM kam alivyokutambulisha katika moja ya ziarani mkiwa Bukoba.
 
Nani aliyetaka kumuhujumu Mama Samia asirithi kiti baada ya mwendazake kukata umeme? Nyie ndio mliotaka kuwachonganisha wananchi!
Source ya hii habari ulipewa na nani?
 
Bashiru ana maadui wengi sana ndani ya chama , hasa kukata mizizi ya wizi ndani ya mikoa na ngazi ya wilaya. Lakini ameonyesha bado ni shupavu na ujengaji wake wa hoja za mantiki ni hazina kubwa aliyonayo. Hata kama kuna mapungufu yalitokea baada ya JPM, bado ninaamini mama atamlinda na amor ubalozi nchi yoyote baada ya miaka hii minne ya ubunge. Kama yeye ni mlangila nina imani hawezi gombea ubunge wa jimbo. Ref, watoto wa Nyerere hamna anayepata ubunge Musoma sababu wazanaki ni minority Musoma , Na kule Bukoba hali kadhalika Mlangila hawezi kupata ubunge licha ya kwamba ni watawala kabla ya uhuru. Kwa intelect yake na uzalendo wake Bashiru atakuwa Balozi huko mbeleni na hasa kwenye utawala wa mama Samia hawezi kumtupa kijana kipenzi wa JPM jamii ya wastaarabu haruwezi kumwelewa na usemi wakazi iendelee ni pamoja na kuenzi mema ya marehemu. Bashiru ndiye kafanya chama kijitegemee kifedha baada ya kuhamishia mapato yote makao makuu. HONGERA Bashiru taifa limefiwa ,lakini mwenzetu meguswa zaidi na kifo cha marehemu , muzilankende mwenzake na JPM kam alivyokutambulisha katika moja ya ziarani mkiwa Bukoba.
Bashiru akiomba ridhaa ya kuwa rais wa Tanzania anashinda mapema sana
 
Kweli kabisa wameshindwa yaani umetoka kuwa karibu mkuu kiongozi Hadi mbunge WA viti maalum
 
Source ya hii habari ulipewa na nani?

Kwanini mlimpangia ziara ya Tanga ili hali kiafya hali ya mwendezake ilikuwa TETE? Huoni kuwa busara ilitakiwa asingekuwa mbali na Mkuu wake?
 
Kwanini mlimpangia ziara ya Tanga ili hali kiafya hali ya mwendezake ilikuwa TETE? Huoni kuwa busara ilitakiwa asingekuwa mbali na Mkuu wake?
Bila shaka wewe ni mmoja ya walioshindwa na kulegea
 
Yeye ndio amepitia kipindi kigumu baada ya Meko kufwa na sio nchi imepitia kipindi kigumu.

Exactly! Apite hivi…..ndio maana baadhi ya wabunge wa kuteuliwa au viti maalum naonaga hawana TIJA ni hasara tu!
 
Bila shaka wewe ni mmoja ya walioshindwa na kulegea

We ngoja hiyo report ya BOT itoke ndio utajua nani atalegea!!! Unafikiri umesamehewa hata kama umerudisha hizo hela mlizoiba!!!
 
We ngoja hiyo report ya BOT itoke ndio utajua nani atalegea!!! Unafikiri umesamehewa hata kama umerudisha hizo hela mlizoiba!!!
Itapuuzwa kama ilivyopuuzwa report ya corona
 
Katibu mkuu msitaafu wa CCM na mbunge wa kuteuliwa Dk Bashiru Kakurwa wakati akichangia hoja kwenye mjadala wa wizara ya kilimo amesema nchi yetu imepitia kipindi kigumu baada ya kuondokewa na aliyekuwa rais wa tano wa nchi yetu hayati Dk Magufuli.

Dk Bashiru amesema kutokana na hali hiyo kuna kundi la watu walijipanga kuwachonganisha watanzania kwa kutunga uongo na kusambaza mtandaoni lakini watu hao wameshindwa na kulegea.

=======

Mbunge wa kuteuliwa, Dk Bashiru Ally amesema majaribio yaliyolenga kuwagombanisha Watanzania yameshindwa na kulegea.

Dodoma. Mbunge wa kuteuliwa, Dk Bashiru Ally amesema majaribio yaliyolenga kuwagombanisha Watanzania yameshindwa na kulegea.

“Nchi yetu imepita katika kipindi kigumu cha kihistoria ambacho hatujawahi kuipitia kutokana na msiba mkubwa uliotukumba, kulikuwepo majaribio ya kutuchonganisha na wakati mwingine kudhalilisha watu na kutunga maneno ya uongo ili nchi itikisike, lakini wameshindwa na wamelegea,” amesema katibu mkuu huyo wa zamani wa CCM.

Dk Bashiru ameeleza hayo bungeni mjini Dodoma leo Jumanne Mei 25, 2021 katika mjadala wa bajeti ya Wizara ya Kilimo ikiwa ni mara yake ya kwanza kuzungumza bungeni tangu alipoteuliwa na Rais Samia Suhulu Hassan Machi 31, 2021.

Bila ya kutaja ni maeneo gani na watu gani waliokuwa wakiwagombanisha Watanzania na kuwazushia uongo, amemshukuru Mungu kwa kuwa Rais Samia na makamu wake, Dk Philip Mpango wameonyesha dira na matumaini ya Tanzania kwa siku za usoni.

Dk Bashiru aliteuliwa kuwa mbunge akiwa amedumu kwa wiki tano katika wadhifa wa katibu mkuu kiongozi baada ya kuteuliwa na Hayati John Magufuli Februari 26, 2021.

Nyoka ya uteuzi kwa Dk Bashiru ilianzia Mei 2018 alipoteuliwa kuwa katibu mkuu wa CCM baada ya kufanya vizuri katika kamati ya kuchunguza mali za chama hicho tawala nchini Tanzania.

Leo katika mchango wake Spika Job Ndugai alimuweka kuwa mchangiaji wa mwisho na kumpa dakika 10 wakati wabunge wengine walikuwa wakipewa dakika tano.

“Mimi ni mteuliwa kati ya nafasi za rais na hadi sasa tupo wanane, nataka nimuahidi rais kuwa sitamuangusha katika nafasi hii aliyoniamini,” amesema huku akiendelea kuchangia kuhusu masuala ya kilimo.

Chanzo: Mwananchi
View attachment 1798472
Bunge lao, wampe hata siku nzima aongee, maana waliomo mle ndani wote wanamshukuru kwa kuwapa ulaji!
 
Back
Top Bottom