Felchesmi Mramba aliwahi kusema PSPF Twin Tower, Uhuru Height na Viva Tower kwa pamoja yanatumia umeme mwingi kuliko ule unaotumiwa na baadhi ya mikoa nchini kama Ruvuma, Manyara, Singida, Kigoma na Rukwa. PSPF peke yake linahitaji megawati tano na Uhuru Height megawati 2.5, Viva Tower megawati 2.5 na Benjamin Mkapa Tower megawati mbili.
Alitaja matumizi ya umeme katika mikoa hiyo na megawati zake kwenye mabano kuwa ni Manyara (10) Mtwara (8), Singida (7), Lindi (5.5), Kigoma (6), Ruvuma (4.7) na Rukwa (6.8).