Mkalukungone mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 862
- 1,755
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko amewahimiza watu wenye ualbino nchini kutembea kifua mbele na kutojiona wanyonge kutokana na hali yao na badala yake watambue kuwa wao ni muhimu kama ilivyo kwa watu wengine.
Dkt. Biteko ametoa rai hiyo Januari 24, 2025 Jijini Dar es Salaam katika hafla ya kugawa vifaa kinga vya saratani ya ngozi kwa watu wenye ualbino pamoja na Uchunguzi wa Saratani ya Ngozi kwa Watu wenye Ualbino.
Amesema tukio la utoaji wa vifaa hivyo ulioratibiwa na Manara TV kwa kushirikikana na chama cha watu wenye ualbino ni kudhihirisha kuwa kuna ushirikiano wa dhati kuunga mkono juhudi za Serikali za kuwasaidia na kuboresha maisha ya watu wenye ualbino nchini.