Uchaguzi 2020 Dkt. Charles Kimei aonesha ukomavu, awashukuru wanachama kwa kumuamini katika hatua ya awali

SautiYaMnyonge

JF-Expert Member
Joined
May 13, 2018
Posts
439
Reaction score
742
Mkurugenzi Mtendaji Mstaafu wa CRDB Dkt Charles Stephen Kimei ambaye alijitosa kutafuta tiketi ya kuteuliwa kuwa mgombea ubunge jimbo la Vunjo kupitia CCM na kupata kura 178 huku mshindi Ndugu Enock Zadock Koola akipata kura 187 amesema anawashukuru wanachama wenzake kwa kumuamini katika hatua hii ya awali.

Na amewaomba kuendeleza umoja na mshikamano ili pale vikao vya uteuzi vitakapokamilisha kazi yake na kutupa mgombea mmoja kwa pamoja tukahakikishe anashinda na CCM inapata ushindi wa heshima kwa ngazi zote.

Kidumu Chama Cha Mapinduzi
 
Hapa ndo ujue kwamba ulimwengu wa wapigakura ni tofauti sana na ile dunia tunaoishi tunaojifanya wasomi na wajuzi wa mambo.

Same same kwa kilichompata ndugu Pasco Mayalla, ujuaji mwingi wa hoja ila wakulungwa wamemkata.

Ila nadhani kamati kuu hapa kwa Kimei lazima wapindue meza
 
Kwa nini wapindue meza?Kama aliyeshika number moja kashinda kihalali ?Kamati kuu huwa wanakata kwa sababu pia,Mara Nyingi wanaoongoza ndo wanapita hata kamati kuu.
 
Mkurugenzi Mtendaji Mstaafu wa CRDB Dkt Charles Stephen Kimei ambaye alijitosa kutafuta tiketi ya kuteuliwa kuwa mgombea ubunge jimbo la Vunjo kupitia CCM na kupata kura 178 huku mshindi Ndugu Enock Zadock Koola akipata kura 187 amesema anawashukuru wanachama wenzake kwa kumuamini katika hatua hii ya awali na amewaomba kuendeleza umoja na mshikamano ili pale vikao vya uteuzi vitakapokamilisha kazi yake na kutupa mgombea mmoja kwa pamoja tukahakikishe anashinda na CCM inapata ushindi wa heshima kwa ngazi zote.

Kidumu Chama Cha Mapinduzi.
Kimei kimei! Mara ooh, wanaogombea na kimei wanapoteza muda wao...Sasa umekuja na ngonjera nyingine! Mfyuuuu!
 
Ila wachaga hawaangali pesa wala vyeo. Ingekuwa Bariadi kwetu basi Kimei angeshinda asubuhi. Chenge alitoka Dar akaja akashinda kirahiiiiisi.
Nahisi hapa labda wapindue meza. BTW ameshindwa pia kwa kura chache, kwa hiyo hata wakipundua meza kuna justification wanaweza toa.

Lakini muda mwingine huwa nawashangaa wapiga kura kumtosa mtu kama Kimei (Phd Holder in Economics, Corporate leader) hawa ndo watu wa kupigiwa kura jamani
 
Mkurugenzi Mtendaji Mstaafu wa CRDB Dkt Charles Stephen Kimei ambaye alijitosa kutafuta tiketi ya kuteuliwa kuwa mgombea ubunge jimbo la Vunjo
Mzee Kimei, kama tungekutana na wewe tena kama ili vyokuwa siku ile pale koridoni nisingekushauri kugombea ubunge. Anyway, kwa neema za Mungu naamini tutaonana tena kwenye kahawa yetu pale pa siku zote
 
Ila wachaga hawaangali pesa wala vyeo. Ingekuwa Bariadi kwetu basi Kimei angeshinda asubuhi. Chenge alitoka Dar akaja akashinda kirahiiiiisi.
Hivi Chenge mwaka huu yumo?
 
Kwa nini wapindue meza?Kama aliyeshika number moja kashinda kihalali ?Kamati kuu huwa wanakata kwa sababu pia,Mara Nyingi wanaoongoza ndo wanapita hata kamati kuu.
Basi ndo kwa heri yake... ila lakini aliyeshinda huwezi jua ana nini cha ziada.. usilolijua ni usiku wa giza, huenda anawafaa waliomchagua
 
Hapa ndo ujue kwamba ulimwengu wa wapigakura ni tofauti sana na ile dunia tunaoishi tunaojifanya wasomi na wajuzi wa mambo.

Same same kwa kilichompata ndugu Pasco Mayalla, ujuaji mwingi wa hoja ila wakulungwa wamemkata.

Ila nadhani kamati kuu hapa kwa Kimei lazima wapindue meza
Kwa kimei laziiiiimaaaaaa meza ipinduliwe. Huyu anarudi
 
Hapa ndo ujue kwamba ulimwengu wa wapigakura ni tofauti sana na ile dunia tunaoishi tunaojifanya wasomi na wajuzi wa mambo.

Same same kwa kilichompata ndugu Pasco Mayalla, ujuaji mwingi wa hoja ila wakulungwa wamemkata.

Ila nadhani kamati kuu hapa kwa Kimei lazima wapindue meza
Koola si light weight nadhani ni mtoto wa Zadock Koola yule jamaa wa ZK Advertisement! Kimei ana chance ya kupewa Ubunge wa kuteuliwa maana nilishamsikia JPM akimpamba kiaina!
 
Ila wachaga hawaangali pesa wala vyeo. Ingekuwa Bariadi kwetu basi Kimei angeshinda asubuhi. Chenge alitoka Dar akaja akashinda kirahiiiiisi.
Pesa wachaga wanazo infact sio washamba wa pesa....
ukiangalia kwa undani sana wachaga wana utu wanadeal na mtu wanayemuamini
 
Nahisi hapa labda wapindue meza. BTW ameshindwa pia kwa kura chache, kwa hiyo hata wakipundua meza kuna justification wanaweza toa.

Lakini muda mwingine huwa nawashangaa wapiga kura kumtosa mtu kama Kimei (Phd Holder in Economics, Corporate leader) hawa ndo watu wa kupigiwa kura jamani
Hao waliopiga kura wanazijua hizo PHD zake kwamba zitawasaidiaje kwenye jimbo?
 
Back
Top Bottom