Zanzibar-ASP
JF-Expert Member
- Nov 28, 2013
- 11,550
- 40,697
Nini maana ya kupiga kura ili kumpata mshindi?Nahisi hapa labda wapindue meza. BTW ameshindwa pia kwa kura chache, kwa hiyo hata wakipundua meza kuna justification wanaweza toa.
Lakini muda mwingine huwa nawashangaa wapiga kura kumtosa mtu kama Kimei (Phd Holder in Economics, Corporate leader) hawa ndo watu wa kupigiwa kura jamani
Hata Kimei angeachwa kwa kura moja tu, bado atakuwa ameshindwa. Ni vyema aliyeshinda akaheshimiwa na kupewa haki yake ya kugombea.
Kuhusu Elimu na umaarufu, kwenye kura za maoni sio kigezo kabisa, na huwa hakiangaliwi kabisa na wajumbe wa CCM.
Kuna mamia ya wasomi na watu maarufu kama Kimei wameangukia pua. Kwanini upendeleo uwe kwa Kimei tu?
Jiulize tu hili swali, Kimei ameifanyia nini CCM Vunjo mpaka awe mgombea wao?
Yote kwa yote, kwangu ningependekeza kuwa mahali popote ambapo mshindi ameongoza kwa tofauti ya kura chache, basi kinyang'anyiro kirudiwe tena, wagombea wasiozidi watatu wenye kura nyingi ndio washindane.