Uchaguzi 2020 Dkt. Charles Kimei aonesha ukomavu, awashukuru wanachama kwa kumuamini katika hatua ya awali

Inavyoelekea ata angeshinda wangemkata juu kwa juu, kwenye interview yake Dr Bashiru ilikuwa keshaanza kumrushia dongo alianza na kujitolea mfano yeye kuna watu tukishapewa nafasi fulani kugombea zingine inakuwa aiwezekani tena baada ya kumaliza muda wetu.

Wakati anataka kuendelea sasa unakuta mtu keshakuwa mkurugenzi lakini....akawa disrupted na swali lingine, inaonekana wangemlimia mbele ata angeshinda kura za maoni.

Ingelikuwa kweli anataka siasa angeachia nafasi yake CRDB kabla ya umri wa kustaafu akagombea ubunge; unasubiri pepo ipotee ndio ujifanye unajali it doesn’t work that way regardless how qualified he is.
 
Siasa za bongo kujuana watu hawaangalii uwezo wala CV ya mtu.Yaani kama hujuani na wajumbe basi huchaguliwi.

Ndugu yangu Mayala nae kalala na viatu,japokuwa maarufu humu JF,CV nzuri ila wajumbe wenye CCM yao hawakujui.
 
huyo mangungu ana kasoro gani?Ilitakiwa wampe nani?
Mangungu alishawahi kuwa mbunge 2010..2015 wananchi hawakuona cha maana alichofanya 2015..2020 wakapeleka jimbo upinzani kwa makusudi...... Leo hii kwa tamaa ya pesa walonayo wajumbe wa mkutano mkuu wilaya wamenunuliwa wamempitisha yule yule asiyekubalika
 
ooh hapo kweli wamefanya utopolo
 
Ila wachaga hawaangali pesa wala vyeo. Ingekuwa Bariadi kwetu basi Kimei angeshinda asubuhi. Chenge alitoka Dar akaja akashinda kirahiiiiisi.
Ulizia The Late Paul Bomani vs Pascal Mabiti , au Jumanne Malecele vs Kibajaji
 
Ahamishie turufu yake ACT
 
Wabunge ni wawakilishi wa wananchi. Inatakiwa mbunge awe mmoja wenu, mwenye kuelewa mahitaji yenu, maisha yenu, na mwenye kuwa na interest zenu moyoni. Sio mtu anayeishi kama malaika, utegemee anakumbuka maisha ya kishetani yalivyo hata kama alitokamo humo.
 
Amefuata nyayo za Makonda za kushukuru wananchi hata ukishindwa
 
Kimei lazima atinge bungeni either kwa Kuchaguliwa au kwa kuteuliwa nahisi Phd nyingi zimekimbilia majimboni kama kina Ndalichako, Philip Mpango, Kabudi n.k ivo mzee baba katika zile nafasi zake 10 za wabunge atavuta PHD nyingine ili Cabinet yake ishibe Wasomi kuanzia Naibu mpaka Waziri
 
Huyu ametafuta kujidhalilisha tu
 
Ila wachaga hawaangali pesa wala vyeo. Ingekuwa Bariadi kwetu basi Kimei angeshinda asubuhi. Chenge alitoka Dar akaja akashinda kirahiiiiisi.
Wewe ni wa Bariadi au Gitega?
 
Itakua sio sawa

Kwa calliber yake alitakiwa awe mshindi wa kishindo

Wakaazi wa kule hawamtaki
 
Unawez akuanmaarufu nchini lakini anayekupita kwa kura ni maarufu jimboni kwa mchango wake ki utendaji
 
Ila wachaga hawaangali pesa wala vyeo. Ingekuwa Bariadi kwetu basi Kimei angeshinda asubuhi. Chenge alitoka Dar akaja akashinda kirahiiiiisi.
Kwenu Moshi pesa mbele Mama. Chenge ni maarufu na wanamuamini bila hata ya pesa. Hawafahamu makandokando yake. Kimei yawezekana hakucheza rough ndiyo maana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…