Dkt. Charles Kimei: Bunge liwajibike kusimamia bajeti inayotekeleza kwa asilimia 100%

Dkt. Charles Kimei: Bunge liwajibike kusimamia bajeti inayotekeleza kwa asilimia 100%

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,880
Reaction score
6,368
Mbunge wa Vunjo, Dkt. Charles Kimei amesema Bunge lazima liwajibike katika kusimamia Serikali ili ije na Bajeti ambayo inatekelezeka kwa asilimia 100 huku ahadi zinazotolewa nazo zikitekelezwa.

Ameeleza, "Mimi nilikuwa najua Bajeti ni Sheria, lakini kama tupo hapa miezi mitatu halafu tunaambiwa imetekelezwa kwa asilimia 50. Nani anashikwa na kupelekwa kortini? Nani anawajibika kwa hilo?"
 
Tatizo bajeti yenyewe inategemea sana misaada kutoka nje hao wafadhili wasipotoa fedha ndio inakuwa kama hivyo. Kuna mwaka nilisikia zito kabwe analalamika Bungeni kwamba wapo kwenye Bunge la Bajeti ambapo bado kama mwezi Bajeti ya Mwaka iishe kuna wizara hadi wakati huo imeshapelekea 30% tu ya bajeti ambao walipitisiwa mwaka uliopita halafu liwaziri husika lipo kimya tu hata halilalamiki.

Ifike wakati hii Nchi isiwe na bajeti wala Bune la Bajeti manake aina maana yeyote. Eti utasikia mawaziri yanasifia eti Bajeti imeongezeka kutoka kiasi fulani hadi kiasi fulani wakati kwenye utekelezaji hicho kiasi hakipelekwi kwenye wizara husika.

Kiufupi hawa wanasiasa wa CCM wanaidanganya sana hii nchi inabidi wachukuliwe hatua za kisheria kama alivyoshauri kimei
 
Kama anasimamia ukweli, basi atoe shilingi kwenye bajeti za Wizara zembe
Hoja siyo kutoa shilingi, ni upuuzi wa kukaa miezi mitatu kujadili kitu ambacho hakifanyiwi kazi.
Kwa nini bunge na taifa Zima kujidanganya?
 
Huyu angepewa Wizara ya Fedha huenda tungefanya jambo kuliko Waziri aliyepo saivi maana hana tofauti saana na Sabaya
Bajeti si ni makararasi tu ya kutumia ulichokusanya sasa Kama hukusanyi huna cash utakuwa na miujiza kutekeleza
 
Kimei angepumzika tu what a disappointment akiwa kama top economist and a succeful banking career spanning over 30 years at top manangement.

I had high hopes kwa experience yake atoe ushauri wa sustainability ya mapato serikalini, kushauri kwenye investment zenye tija na high yield za kiuchumi etc to do with elimu yake na mafanikio yake in the banking.

Labda kweli ukiingia CCM akili unatakiwa uziache huko huko, yaani amekuwa na michango ya ovyo very simple like an average MP.
 
Kimei angepumzika tu what a disappointment akiwa kama an economist and succeful banker I had hopes kwa nafasi yake atoe ushauri wa sustainability ya mapato serikalini, kushauri kwenye investment zenye tija na high yield za kiuchumi etc to do with elimu yake na mafanikio yake.

Labda kweli ukiingia CCM akili unatakiwa uziache huko huko, yaani amekuwa na michango ya ovyo very simple like an average MP.
We usha wahi kufuatilia michango yake yote Bungeni? Au unaongea uharo tu humu ilimuladi na wewe uonekane umechangia,

Fuatilia michango yake tangu January acha ujinga then rudi humu
 
Mbunge wa Vunjo, Dkt. Charles Kimei amesema Bunge lazima liwajibike katika kusimamia Serikali ili ije na Bajeti ambayo inatekelezeka kwa asilimia 100 huku ahadi zinazotolewa nazo zikitekelezwa

Ameeleza, "Mimi nilikuwa najua Bajeti ni Sheria, lakini kama tupo hapa miezi mitatu halafu tunaambiwa imetekelezwa kwa asilimia 50. Nani anashikwa na kupelekwa kortini? Nani anawajibika kwa hilo?"
Tatizo linaanzia kwa mawaziri ambao serikali ikipeleka fedha kwa kazi yo yote ile wanabaki kumsifia Rais kama vile ametoa fedha zake mfukoni wakati ni kodi zetu!

Oh Rais katoa fedha kujenga zahanati; oh Rais katoa fedha za madawati; oh Rais katoa fedha kujenga mtaro...nk, wabunge kwa ujinga wao wanabaki kushangilia kama mazuzu!

Upuuzi mtupu!
 
Mbunge wa Vunjo, Dkt. Charles Kimei amesema Bunge lazima liwajibike katika kusimamia Serikali ili ije na Bajeti ambayo inatekelezeka kwa asilimia 100 huku ahadi zinazotolewa nazo zikitekelezwa.

Ameeleza, "Mimi nilikuwa najua Bajeti ni Sheria, lakini kama tupo hapa miezi mitatu halafu tunaambiwa imetekelezwa kwa asilimia 50. Nani anashikwa na kupelekwa kortini? Nani anawajibika kwa hilo?"
Mbona yeye hajawajibika kwa madudu aliyofanya CRDB?
 
We usha wahi kufuatilia michango yake yote Bungeni? Au unaongea uharo tu humu ilimuladi na wewe uonekane umechangia,

Fuatilia michango yake tangu January acha ujinga then rudi humu
Taja mchango wake mmoja wenye tija kabla ya kuanza kutukana watu.

Hivi kwanini kuna watu mna midomo michafu sana, tena unakuta without provocation ni malezi au frustrations za maisha.

Hakuna kitu cha maana Kimei ameongea bungeni kama una elewa ni aina gani ya decision alizokuwa anafanya CRDB na reasoning process zake.

He is just plain bungeni, kama huna hoja ya finance au ya kiuchumi please save it ain’t no body interested na mambo ya kutukanana.
 
Dr. Kimei yupo sahihi kabisa. Ni kweli kazi ya bunge ni kuisimamia serikali kitu ambacho hakikuwai kufanyika zaidi ya miaka mitano iliyopita.
 
Hapa pana tatizo la kuelewa nani anasimamia nini. Hivi ni Bunge ndio linasimamia Serikali au ni Chama ndicho kinafanya hivyo. Imefikia wakati Katibu Mkuu wa Chama anawaamuru Mawaziri kufanya yale anayotaka yafanyike na hivyo kuingilia maamuzi ya Serikali. Bunge linawekwa pembeni. Katiba ni muhimu katika kupambanua kadhia hii.
 
Hayo mapendekezo si hata msukuma na kibabaji wanaweza kutuambia.

We expect a financier aende deeper na kudadavua risk associated na current income sources, how each source collection could be improved, ashauri kwenye risk mitigations, provision kwenye makusanyo ili serikali ipange sahihi; etc with a realistic budgeting na uwezo wa Kimei kwenye kuchambua budget kutokana na work experience yake.

Ila yeye Kimei anaongea hoja rahisi rahisi kama wabunge waliofuta posho, he is just a disappointment.
 
Kimei angepumzika tu what a disappointment akiwa kama top economist and a succeful banking career spanning over 30 years at top manangement. I had high hopes kwa nafasi experience yake atoe ushauri wa sustainability ya mapato serikalini, kushauri kwenye investment zenye tija na high yield za kiuchumi etc to do with elimu yake na mafanikio yake.

Labda kweli ukiingia CCM akili unatakiwa uziache huko huko, yaani amekuwa na michango ya ovyo very simple like an average MP.

You are off the point....

Imewekwa hoja hapa lakini ni ajabu wewe unamjadili mtu mtoa hoja Kimei...!!

What's wrong with you ndugu...??
 
Lengo la bajeti inayotolewa na Bunge letu "tukufu" sio kutekelezwa kwa 100%🤣🤸🐒
 
You are off the point....

Imewekwa hoja hapa lakini ni ajabu wewe unamjadili mtu mtoa hoja Kimei...!!

What's wrong with you ndugu...??
Namajadili Kimei kwa sababu I expected more from him, ingelikuwa mmbunge mwingine kapendekeza hayo nisingeshangaa based on their limitations.

Kwa watu wanaofahamu michango yangu Kimei was a finance guru in my books wakati yupo CRDB na nimeshapitia maandiko yake kadhaa akiikosoa banking sector katika ujana wake very sound, realistic and clever; ndio maana sishangai mafanikio yake in banking.

Lakini tangia ameingia bungeni amekuwa just an average MP mwenye kuchukua posho tu.
 
We usha wahi kufuatilia michango yake yote Bungeni? Au unaongea uharo tu humu ilimuladi na wewe uonekane umechangia,

Fuatilia michango yake tangu January acha ujinga then rudi humu
That is your observation, kwamba sometimes Kimei michango yake huwa ni uharo tu.. You are totally free to think that way..

Lakini unasahau jambo moja kuwa, hata wewe kuna watu wanaona michango yako popote pale iwe kazini, kijiweni kwako ama hapa jukwaani (JF) ni uharo mtupu....!!

Tusemeje sasa kwa hili....?

Nothing. Zaidi ya kusema hii ndiyo inayoitwa The right for FREEDOM OF EXPRESSION...!

Kinachokosekana kwenye hili, (labda) u - staha wa matumizi ya lugha...

Hicho ndicho tunacho kosa wengi ukiwemo wewe...!!
 
Back
Top Bottom