Uchaguzi 2020 Dkt. Charles Kimei ndiye habari ya Mjini Vunjo

Uchaguzi 2020 Dkt. Charles Kimei ndiye habari ya Mjini Vunjo

Kuna watu wanaamini kwamba Charles Kimei ataibadilisha Vunjo, sasa imani yao inaegemea kwamba jamaa alikuwa CRDB, na wanaamini pesa alizovuna CRDB zitaenda kuibadilisha Vunjo.

Haya ni mawazo si sahihi kabisa, MO alikuwa na pesa mbona singida bado ni masikini? Rostam alifanya nini Igunga si alikuwa na pesa?

wananchi wa vunjo ni werevu, Charles Kimei hatachukua pesa zake za mafao CRDB akawaletee watu maendeleo, hizi ni ndoto Za mchana, wananchi wa vunjo Wanajua mtu bora anayefaa ni Nani.
Bora uwaelimishe kama mnakumbuka enzi zile za Keenja na jiji na Keenja na Ubunge ilikuwa kama mbingu na ardhi
 
Mrema ndio Mbunge wa vunjo. Mrema ana historia ya uchapa kazi nzuri vunjo na kitendo chake cha kuwa karibu na kumuunga mkono Rais, Dkt. Magufuli kitampa kura kwa sababu ya imani kubwa wananchi walionayo kwa Mhe. Rais kwamba anafanya kazi nzuri. Mrema ameshafanya kazi na Magufuli miaka ya 2010 - 2015 ambapo magufuli alikuwa waziri wa ujenzi na Mrema mbunge wa vunjo walishirikiana kujenga barabara jimboni humo.

Mrema kuteuliwa tena kuwa mwenyekiti wa bodi ya parole kwa kipindi cha pili 2020 - 2023 ni heshima kubwa aliyopewa na magufuli na yeye pekee yake kaingia kugombea ubunge bado kashikilia cheo alichopewa na Rais wengine wote wenye tamaa walitumbuliwa.Miradi mingi ya maendeleo ambayo alianzisha Mrema ilikufa baada ya Mbatia kuteuliwa wananchi wengi wanataka hiyo miradi irudi na anayeweza kuifufua ni Mrema.

Mfano barabara Kawawa-nduoni-kilema-marangu mtoni. Kipindi cha ubunge wa Mrema paliwekwa lami marangu mtoni mpaka kilema na kawawa mpaka nduoni. Lakini Mbatia alivyoingia kwenye ubunge lami hiyo haijaunganishwa nduoni mpaka kilema. Mrema ameahidi kuimalizia
Kama hela ya kujenga barabara alitoa mfukoni kwake sawa ila kama ni kodi zetu asahau yeyote ataechaguliwa gurudumu atulie ale mafao
 
Vunjo hii jimboni kwangu??

Sent from my TECNO LA7 using JamiiForums mobile app

Ndio hali halisi ya Vunjo ya leo, sio Kimei tuu, uko uwezekano mkubwa majimbo yote Moshi yakaenda CCM. Nipo Marangu Falls Kinukamori tunapata moja moto na nyingine baridi.

Wakazi wa huku wengi waliopo Chadema waongo hawataki kusema ukweli wa hali iliyovyo. Kilimanjaro yote, Upinzani kutoka bila jimbo haitokuwa kitu cha ajabu.

Tena kura za Urais wengi wanamtaka Magufuli na sio Lissu. NA HUU NDIO UKWELI, WAKAZI WA KILIMANJARO SEMENI UKWELI MTUPU KINYUME CHAKE NI UWONGO MTUPU. SEMENI UKWELI KWANI MTAKUFA?. UPINZANI NGUVU IMEPUNGUA SANA.
 
Duuuu sawa nguvy imepungua mngekuwa na wateka n kukataa kupokea fomu zao

Sent from my TECNO LA7 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom