Dkt. Chaya: Elimu ya nadharia kwenye vyuo ndio inaleta changamoto ya ajira kwa Vijana

Dkt. Chaya: Elimu ya nadharia kwenye vyuo ndio inaleta changamoto ya ajira kwa Vijana

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Mbunge wa Manyoni Mashariki, Dk Pius Chaya (CCM) alisema tatizo la ajira kwa vijana wanaohitimu vyuo vya kati na vikuu nchini katika ngazi za cheti, stashahada na shahada ni kubwa.

Dk Chaya alisema tatizo lipo si kwa sababu elimu ni mbovu, ila kutokana na mfumo wa elimu ambao mwanachuo anajifunza nadharia na vitendo anatakiwa kujifunza akiwa nje ya vyuo vikuu.

Alisema yeye alikuwa mhadhiri Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) na Chuo Cha Mipango, na kwamba idadi kubwa ya wahitimu, wengine zaidi ya miaka minane, wapo mitaani hawana ajira.

“Vyuo vinatoa elimu ya nadharia na namna ya kufanya wanaweza kupata taaluma hiyo kupitia programu mbalimbali ikiwemo inayotolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka mmoja ya kuwasaidia vijana kuwapa ujuzi na uzoefu,” alisema.

Dk Chaya alisema mpango huo wa ofisi ya Waziri Mkuu, unawaandaa vijana na kuwapa Sh 150,000 za kujikimu kwa mwezi, unaweza kupanuliwa na kuwaandaa vijana na kuunganisha na taasisi zinazotafuta watu wa kuajiri.

Alisema vijana hao pia wanaweza kupewa ujuzi na wakaziba pengo la uhaba nafasi wa ajira katika sekta ya afya na elimu kwa kuwapa fedha hizo, badala ya kuwaacha vijana hao mitaani.
 
Back
Top Bottom