Zee la madawa
JF-Expert Member
- Nov 28, 2022
- 1,895
- 4,478
Kwanini Ndg. Omar Kashera alikuwa anachekekea simuliza za ukatili za Omar Mahita wakati wa mahojiano?
Nimemfahamu Omar Kashera mitandaoni na nimekuwa mfuatuliaji mkubwa wa masomo yake ya Diplomasia na Uongozi. Nimekuwa namkubali sana. Lakini nilipofuatilia mahojiano yake na IGP wa zamani Omar Mahita, kuna jambo limenitafakarisha sana. Kila wakati Omar Mahita alikuwa akitoa kauli zinazoashiria ukatili akiamini ndio usahihi, na Ndg Omar Kashera alikuwa akichekelea na kuingiza vineno vya kukubaliana na Mahita. Binafsi hili limenipa wakati mgumu.
Kwa wasiomjua Omar Mahita, anasifika kwa kuwa mtu katili sana, na zaidi ni wale askari wa CCM waliotumika kuhujumua demokrasia kwa maslahi ya CCM. Wakati CUF kikiwa chama cha upinzani, Omar Mahita akiwa IJP alikishughulikia sawasawa. Wafuasi wa CUF walikuwa wakipigwa na kubambikiwa kesi. Siku chache kabla uchaguzi mkuu wa mwaka 2000, Mahita aliita vyombo vya habari na kuonesha visu vyenye alama ya CUF na kuwatangazia watanzania eti jeshi la polisi limekamata silaha za wafuasi CUF waliopanga kufanya fujo. Mahita alikuwa mwanaCCM aliyepewa uongozi wa jeshi la polisi ili ailinde CCM kama ilivyo sasa hivi. Si ajabu Mahita angekuwa IJP leo hii, matukio ya kuteka, kuua, kubambika kesi wapinzani yangekuwa maradufu.
Mahita ni kielelezo cha ukatili wa askari wa jeshi la polisi. Ndio wale watu wenye uwezo mdogo wa kufikiri wanaotumia mabavu zaidi kuliko akili kama askari wengi wa jeshi la polisi.
Kwanini Omar Kashera alikuwa akichekelea simulizi za ukatili za Omar Mahita?
Je! Omar Kashera ni msomi na mwanadiplomasia mzuri wa kichwani na lakini moyoni ni mtu tofauti?
Je! Omar Kashera hana nguvu ya kusimamia anachokiamini hasa akikutana na watu waliomzidi nyadhifa?
Kwanini Omar Kashera alikuwa akichekelea simulizi za ukatili za Omar Mahita, na hata kuchomekea vijineno vya kukubaliana naye?
Nelson Mandela aliwahi kusema; 'Wale wanaoamimi katika utu, maadili na uthabiti, hawapaswi kuhofia uovu na ukatili".
Kama tafsiri yako ya maadili inatofautiana baina ya mtu na mtu, huna maadili.
Nawasilisha!
Dr. Chris Cyrilo.