TANZIA Dkt. Cyril Chami afariki dunia

TANZIA Dkt. Cyril Chami afariki dunia

Informer

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2006
Posts
1,606
Reaction score
6,672
Aliyewahi kuwa mbunge wa Moshi vijijini na Mhadhiri wa UDOM, Dr. Cyrili Agusti Chami amefariki saa 8 usiku wakuamkia Leo Mjini Dodoma.

Bwana ametoa, Bwana ametwaa!

===
FB_IMG_1604553550335.jpg

Dkt. Cyril Agustino Chami amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika Hospitali ya Benjamini Mkapa, Dodoma alikokuwa amelazwa kwa matibabu

Dkt. Chami aliwahi kuwa Mbunge wa Moshi Vijijini kupitia CCM, tangu 2005. Januari 2006 aliteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa

Februari 2008 aliteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko na alikuwa Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko mwaka 2010 hadi 2012.

Hadi mauti yanamkuta, Dr. Chami alikuwa Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) katika Idara ya Uchumi.

Msiba upo nyumbani kwa marehemu Nzuguni.
 
R.I.P kwake! Inna Lillahi wa inna ilayhi raji'un.
 
Dom kuna hospitali nzuri zaidi ya Dar au ni nyumbani kwake?
 
RIP Mbunge, Waziri, Mhadhiri. Poleni wote mlioguswa na msiba huu. Amen
 
Back
Top Bottom