Chizi Maarifa
JF-Expert Member
- Jul 29, 2013
- 10,931
- 24,816
Nachompendea huyu Aunt ni uwezo wake wa kufuatilia mambo kwa ukaribu, of course kipindi kile cha Corona kuna mambo alichemka kama binadamu lakini kwa sasa anafanya kazi ambayo inatakiwa kupongezwa.
Dkt. Gwajima D akili alikuwa nayo basi tu alikuwa na Naibu kilaza ambaye ameendelea kuwa kilaza kwenye mambo mengi anayoyafanya mpaka sasa tofauti na Dkt. Gwajima D ambaye yeye amejifua na kujifunza kuwa smart.
Napendelea utendaji wake wa sasa ambao hauna kelele ila tu una kishindo. anafuatilia kila jambo kwa umakini na pasipo kuwa na kelele.
Nimeangalia hata humu ndani kunapokuwa na jambo hasiti kujitokeza na kujumuika Jukwaani bila woga. Mawaziri na Wabunge wengi hupaogokwa JF na wengi walikimbia baada tu ya kupata vyeo au nafasi mbalimbali. Huyu amekuwepoo na anashiriki debates pasipo woga kabisa.
Mimi naona ni mtu anayefaa sana kuendelea kuwa kiongozi kwa kuwa ana tabia ya kufuatilia jambo kwa kina na majibu ambayo anayatoa sasa mara nyingi ni ya kitaalamu na si ya kisiasa.
Tuendelee kumsadia kwa kumshauri na kumkosoa pale inapobidi ili mambo yaweze kwenda sawa kwa upande wake na kuendeleza uchapaji kazi mzuri.
Pia soma PONGEZI: Utenguzi wa Mkurugenzi Mafia Ili kupisha Uchunguzi, Pongezi ziende kwa Dkt. Dorothy Gwajima. Kiukweli kwenye hili amejituma sana