UMUGHAKA
JF-Expert Member
- Sep 1, 2021
- 2,753
- 12,932
Nsikuchoshe na Usinchoshe, Tusichoshane!
Kwanza kabisa nipende kukiri hadharani ya kwamba,Binafsi huyu ndiye waziri ninaye mkubali Kwa Sasa nchi Tanzania.
Huyu waziri anazosifa kadhaa ambazo zinamfanya aendelee kukubalika Kwa Watanzania kibwena.
SIFA ZINAZOMFANYA KUPENDWA NA WATANZANIA WALIO WENGI
1. Ni mzuri wa Sura na Umbo (Uzuri wake unaendana na Roho yake nzuri)
2. Siyo mtu wa kujikweza
3. Siyo mtu wa dharau kama walivyo mawaziri wengine
4. Mpenda haki
5. Siyo mtu wa hasira za Kijinga
6. Anapenda kusikiliza kila mtu (Ukipitia kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii unakuta anajibu komenti za wananchi Kwa upole na nidhamu ya hali ya juuu,hata kama ukiwa umekwazika utashusha hasira zako)
7. Anachukia sana uovu na Uonevu
8. Ni mtu ambaye madaraka hayajamfanya akengeuke kama mawaziri vishoka wengine!
9. Siyo mtu wa kuongea ongea sana Bali ni mtendaji sana kitu amabacho kinafanya kazi zake ziongee sana kuliko Mdomo wake kama walivyo mawaziri wengine wapiga zomari
Yaani kiukweli nikiamua kuziweka hapa Sifa zake ni nyingi mno,itoshe kusema hapa Rais Samia alitutendea haki watanzania.
Ningekuwa Rais Samia au Mshauri wake,nadhani huyu angetufaa Kuwa WAZIRI WA MAMBO YA NDANI
Nadhani pia ukarimu wake na hofu ni matokea Bora ya kumuabudu Mungu,huyu mama anamuabudu Mungu katika roho na kweli,siyo kama waigizaji wengine walioko kwenye Baraza la mawaziri.
Hongera sana Mh Dkt. Gwajima D