Dkt. Dorothy Gwajima ndiye waziri anayekubalika kwasasa nchini Tanzania

Dkt. Dorothy Gwajima ndiye waziri anayekubalika kwasasa nchini Tanzania

Huyu Bi Mkubwa kiukweli anawatendea haki watanzania,Binafsi ndiye alifaa Kuwa Rais wa hii nchi!
Na hii ndo ilikuwa point yako 😂

Urais ni ahadi toka kwa mungu muumba Kaka... Akishapanga itakuwa tu! Utumie nguvu na usitumie, itakuwa tu!

Ni kweli Mama Dkt. Gwajima D anafanya vyema ingawa bin-Adam hatuishiwi na ya kusema, ila kwa kumpamba sana mpaka kumpa hadhi ya juu kuzidi aliyeko kwenye kiti ni ukosefu wa adabu na chuki binafsi.

Wanawake saiv ni game changers! Kongole kwao, ila pia baadhi yetu/yenu tunatumia/mnatumia nguvu nyingi sana kuwapa sifa na hadhi hadi wasizostahili na kuwa-disvalue wanaume.

HIYO SIO SAWA!
 


Nsikuchoshe na Usinchoshe, Tusichoshane!


Kwanza kabisa nipende kukiri hadharani ya kwamba,Binafsi huyu ndiye waziri ninaye mkubali Kwa Sasa nchi Tanzania.

Huyu waziri anazosifa kadhaa ambazo zinamfanya aendelee kukubalika Kwa Watanzania kibwena.

SIFA ZINAZOMFANYA KUPENDWA NA WATANZANIA WALIO WENGI
1. Ni mzuri wa Sura na Umbo (Uzuri wake unaendana na Roho yake nzuri)

2. Siyo mtu wa kujikweza

3. Siyo mtu wa dharau kama walivyo mawaziri wengine

4. Mpenda haki

5. Siyo mtu wa hasira za Kijinga

6. Anapenda kusikiliza kila mtu (Ukipitia kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii unakuta anajibu komenti za wananchi Kwa upole na nidhamu ya hali ya juuu,hata kama ukiwa umekwazika utashusha hasira zako)

7. Anachukia sana uovu na Uonevu

8. Ni mtu ambaye madaraka hayajamfanya akengeuke kama mawaziri vishoka wengine!

9. Siyo mtu wa kuongea ongea sana Bali ni mtendaji sana kitu amabacho kinafanya kazi zake ziongee sana kuliko Mdomo wake kama walivyo mawaziri wengine wapiga zomari

Yaani kiukweli nikiamua kuziweka hapa Sifa zake ni nyingi mno,itoshe kusema hapa Rais Samia alitutendea haki watanzania.

Ningekuwa Rais Samia au Mshauri wake,nadhani huyu angetufaa Kuwa WAZIRI WA MAMBO YA NDANI

Nadhani pia ukarimu wake na hofu ni matokea Bora ya kumuabudu Mungu,huyu mama anamuabudu Mungu katika roho na kweli,siyo kama waigizaji wengine walioko kwenye Baraza la mawaziri.

Hongera sana Mh Dkt. Gwajima D
Kisa upepo wa waliotumwa na Afande au Kuna jingine? 😁😁
 
tumtafutie Jimbo la kugombea 2025 ili awe mbunge kamili sasa aendeelee na nafasi yake. Tumpe Jimbo la kaka yake pale kawe
 
Dalali wa mbuga atampiga chini sasa hivi.

Mapambio anataka yawe yake tu.
Mkuu una kiona mbali.

Maana tukifurahishwa na teuzi flani na tukapaza sauti kuunga mkono kuwa 'hili sasa ni jembe', muda huo huo utenguzi unafuata ama kubadilishiwa Wizara!

Ref to: 'Uenezi' wa Makonda, Uwaziri wa aridhi wa Slaa, Uwaziri wa nishati wa Kalemani na baadhi yao ambao sijawakumbuka!

Kumbe inatakiwa sifa na utukufu zimwendee yeye pekee?
 
Hakika Ni wazir ambaye ameamua kuwa karbu zaid na raia. big up Dr Gwajima
Na ndio inapaswa kiongozi kuwa karibu na watu wake, ukaribunna raia ndo utajua Nini wanachi wanataka sio kiongozi unataka... Citizen voice is national voice cause are ones with needs not leaders 😊
 
Naunga mkono hoja anastahili sijui kwann walimuondoa afya kule Kuna upuuzi mwingi sana unafanyika.
 
Back
Top Bottom