Pre GE2025 Dkt. Emmanuel Nchimbi ateuliwa kuwa Katibu Mkuu mpya wa CCM kumrithi Daniel Chongolo

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Kazi iendelee. CCM Ni taasisi imara inayoendelea kuonyesha ukubwa wake,ukomavu wake na umadhubuti wake katika kujiendesha kitaasisi na kufanya mambo yake kisayansi na kisasa. Sasa kazi ya kukiandaa chama iendelee katika kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa pamoja na uchaguzi mkuu mwaka kesho ili chama kipate ushindi wa kishindo katika kila ngazi ya uchaguzi,hasa kwa kuzingatia ukweli kuwa vyama vya upinzani hapa nchini vikiongozwa na CHADEMA ni dhaifu na havina sera wala ajenda za kugusa maisha ya watanzania kuweza kuaminiwa na kupewa kura za ndio.
 
rekebisha hapo pa kufikisha miaka 44 mwishoni mwa mwaka
 
Tuna imani na Dr Emmanuel Nchimbi kutuvusha na kufanya kazi za utendaji mkuu wa chama chetu .chama kimewekwa katika mikono sahihi kiutendaji.kimewekwa mikononi mwa mtu na kiongozi mchapa kazi na mwenye uzoefu wa hali ya juu sana kitaifa na kimataifa serikalini na chamani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…