Pre GE2025 Dkt. Emmanuel Nchimbi: Mwenyekiti wetu amefanya mambo makubwa bila majivuno. Angekuwa mwingine kafanya hakuna rangi tungeacha kuiona

Pre GE2025 Dkt. Emmanuel Nchimbi: Mwenyekiti wetu amefanya mambo makubwa bila majivuno. Angekuwa mwingine kafanya hakuna rangi tungeacha kuiona

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
naona vita marehemu inaendelea.

Mwambieni Nchimbi, kwa maneno hayo tu hafai tena kuitwa Dr.. tutamuita kwa jina lake Emmanuel Nchimbi.

Tutampima na kuwapima kwa matokeo ya kazi yao na sio blah blah, vijembe na taarabu.
 
Kwanza Kila siku nawaambia humu kwamba Mimi sio mwanaccm Bali shabiki tuu wa Samia.

Pili sijawahi sifia kitu ambacho Rais hajafanya Kwa sababu sitafuti nafasi Bali ni sehemu ya proudness of her leadership amewashinda Wanaume ambao Huwa wanajifanya Wana akili.

Mimi sio tuu nasifia Bali Huwa nakosoa inawezekana wewe hunifahamu.

Mwisho Kwa umri wangu Toka nimeanza kufuatilia siasa Rais pekee ambae anatambua shida za watu na namna ya kuzitatua ni Samia.

-Samia ndio ameweka Nguvu kubwa kumtua mama ndoo kichwani Kwa sababu anatambua adha ya Wanawake
-Samia ndio ameweka Nguvu kubwa kwenye Kilimo Kwa sababu anatambua kamba Asilimia 65% ya Watanzania ni wakulima na 90% ya Ajira zinatoka kwenye Kilimo.
-Samia ndio ametatua shida ya Barabara za Vijijini ndio maana husikii kelele ameongeza Bajeti mara 5
-Samia ndio ameweka Nguvu kubwa kwenye Afya ambako akina mama wenzie wanapata shida
-Samia ndio amelenga kuwainua wanawake kutoka kuzuiwa shida kisa mimba Hadi kuwarejesha shule na Kuwajengea shule maalumu za bwawni za Wanawake Nchi nzima nk

Kiufupi Samia anajua wapi Kuna shida na wapi aweke Nguvu,wale wengine walikuwa hawajitambui na wanatafuta vitu cheap Ili wapate sifa kama kujenga reli,ndege na madaraja makubwa hata kama Yana Tija ndogo Kwa watu.
Ushasema wewe ni shabiki wa Samia na hata huko kukosoa unakozungumzia huwa humkosoi Samia huwa unakosoa mambo ambayo hayamuhusishi Samia.

Hivyo unavyomuona wewe Samia kwamba ni bora na kafanya makubwa kuliko wote waliyomtangulia ni katika sehemu ya ushabiki wako kwake tu japo hilo wewe huwezi kuona au kukiri, kama ambavyo waliyomshabikia Magufuli na wapo mashabiki wa Kikwete na Mkapa hadi leo.

Kwangu mimi kumsifia kiongozi si tatizo ila inapofikia hali hadi ya kushindwa kumkosoa penye makosa au kutotaka akosolewe huo unakuwa ni upuuzi na bora anayefanya hivyo kimasilahi naweza kumuelewa kuliko anayefanya hivyo kiushabiki tu aweza kuwa hata ana matatizo ya akili.
 
Namba ndio zinaongea sio porojo zenu

View: https://www.instagram.com/p/C2QQGqssLrP/?igsh=MWZlYzllZW56YXdpbA==
 
Mambo gani yangu yaende wakati hakuna anaenifahamu huko ccm? Kimsingi nafurahia Kwa kuturejeshea thamani ya Kilimo ,Mimi ni mkulima naona tofauti kutoka kukosa soko Hadi kupata soko zuri.
Narudia tena mkuu kuwa hii nchi ni kubwa na ina matatizo sugu mengi tu, wewe kama shabiki wa Samia na sie tusio mashabiki lazima tutofautiane mitazamo. Wewe unamtazama Samia anayofanya na kupambwa nayo ndio maana hata serikali ikinunua madawati kwako ni jambo kubwa na sifa kwa Samia ila wengine tunatizama nchi kwa ujumla wake.
 
Serikali zenu za 🌈 zilifanya yapi ya maana zaidi ya kusumbua awamu za Waislamu?
 
Kumbuka mkuu hiyo ni serikali na hayo majukumu yake ya kawaida tu na sio msaada wa Bakhresa au Mo hapo, sasa sijui cha ajabu unachotaka kutushangaza sisi ni kipi?
Majukumu ya kawaida ila Kwa Kasi kubwa kushinda zingine,that is the point.

Unaweza maliza mbio ila usimalize Kwa wakati na mwingine.

Samia anawapelekea Moto 🌈
 
Back
Top Bottom