Dkt. Emmanuel Nchimbi: Nililipiwa ada na Hayati Mkapa. Nasikitika kutohudhuria mazishi yake

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2022
Posts
28,722
Reaction score
20,610
Ndugu zangu Watanzania,

Katibu Mkuu wa CCM Dkt Emmanueli Nchimbi Ametua kusini Rasmi kuanza na kuendelea na ziara yake ya kichama kama ambavyo niliwajuzeni humu jukwaani. Ambapo ameambatana na wajumbe wa sekretarieti akiwepo katibu wetu Mwenezi CCM Taifa Ndugu CPA Amos Makala.

Ambapo katibu Mkuu wetu ameweza kufika katika Nyumba ya milele ya Hayati Benjamini Mkapa Rais wa awamu ya Tatu wa Tanzania,aliyefariki Mwaka 2020 Julai 24 na kuzikwa Julai 29 nyumbani kwake Lupaso. Ambapo katibu wetu ameeleza mengi sana juu ya uhusiano wake mzuri na Hayati Benjamini Mkapa na namna alivyofanya naye kazi kwa takribani miaka saba.

Ambapo Balozi Dkt Emmanueli Nchimbi Amesema ya kuwa siku Moja aliitwa na Hayati Mzee Mkapa akaulizwa juu ya Elimu yake ,ambapo alijibu kuwa ana shahada moja tu. Akasema kuwa akamwambia Elimu hiyo haitoshi kwa Mwenyekiti wa UVCCM Taifa .Ambapo Akaulizwa kwanini hajaendelea na masomo ya juu zaidi. Akajibu kuwa hana ada.

Balozi Dkt Emmanueli Nchimbi ameendelea kusema kuwa baada ya jibu hilo mazungumzo yakaishia hapo ,ambapo hata hivyo baada ya siku chache aliitwa na mtu ambaye alimwambia kuwa kuna barua yake kutoka kwa Rais.na alipokutana na mtu huyo alimweleza ya kuwa Rais amefanya utafiti na uchunguzi na kugundua vyuo vya Mzumbe na Chuo kikuu cha Dar ada zake hazizidi million mbili na hivyo achukue hela akalipe ada ili aendelee na masomo.

Hata hivyo Balozi Dkt Emmanueli Nchimbi amesikitika na kuumia sana kukosa mazishi ya kiongozi huyo anayekumbukwa kwa kuanzisha Taasisi mbalimbali hapa Nchini ambazo zinaendelea kufanya vyema sana.taasisi hizo ni kama vile TRA na zingine nyingi sana.

Anasema sababu ya kushindwa kuhudhuria ni kwa kuwa wakati huo kulikuwa na ugonjwa wa Corona ,ambapo viwanja vilikuwa vimefungwa na hivyo akashindwa kusafiri kuja Nchini kushiriki Mazishi,anasema kuwa ndio maana alipofika tu nchini alikwenda moja kwa moja kwa Mama Anna Mkapa Kumpa pole. Na kwamba leo anayo furaha kutembelea mahali alipo lala Hayati Benjamini Mkapa.

Baada ya kusikia maneno hayo Mimi Mwashambwa nimeona kuwa Inaonyesha Hayati Mzee Benjamin Mkapa alikuwa na moyo mzuri .maana nakumbuka kama sijakosea hata Mheshimiwa Ridhiwani Kikwete amewahi kusema hadharani kuwa alilipiwa ada na Hayati Mkapa.

Rai yangu ni kuwaomba viongozi na wote wenye uwezo na nafasi ya kifedha kuweza kusaidia wenye uhitaji na wasio na uwezo. Siyo tu kwa wale wanaowafahamu bali hata kwa wale ambao hawawafahamu lakini wamewaona kuwa wana shida na uhitaji.

Mwisho naendelea kuwakumbusha kwa maneno haya kutoka kwenye Biblia ndugu zangu. Kwa kila jambo na majira yake na wakati kwa kusudi maalumu chini ya mbingu.

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Screenshot_20240728-144051_1.jpg
 
Ndugu zangu Watanzania,

Katibu Mkuu wa CCM Dkt Emmanueli Nchimbi Ametua kusini Rasmi kuanza na kuendelea na ziara yake ya kichama kama ambavyo niliwajuzeni humu jukwaani.Ambapo ameambatana na wajumbe wa secretarieti akiwepo katibu wetu Mwenezi CCM Taifa Ndugu CPA Amos Makala.

Ambapo katibu Mkuu wetu ameweza kufika katika Nyumba ya milele ya Hayati Benjamini Mkapa Rais wa awamu ya Tatu wa Tanzania,aliyefariki Mwaka 2020 Julai 24 na kuzikwa Julai 29 nyumbani kwake Lupaso. Ambapo katibu wetu ameeleza mengi sana juu ya uhusiano wake mzuri na Hayati Benjamini Mkapa na namna alivyofanya naye kazi kwa takribani miaka saba.

Ambapo Balozi Dkt Emmanueli Nchimbi Amesema ya kuwa siku Moja aliitwa na Hayati Mzee Mkapa akaulizwa juu ya Elimu yake ,ambapo alijibu kuwa ana shahada moja tu. Akasema kuwa akamwambia Elimu hiyo haitoshi kwa Mwenyekiti wa UVCCM Taifa .Ambapo Akaulizwa kwanini hajaendelea na masomo ya juu zaidi. Akajibu kuwa hana ada .

Balozi Dkt Emmanueli Nchimbi ameendelea kusema kuwa baada ya jibu hilo mazungumzo yakaishia hapo ,ambapo hata hivyo baada ya siku chache aliitwa na mtu ambaye alimwambia kuwa kuna barua yake kutoka kwa Rais.na alipokutana na mtu huyo alimweleza ya kuwa Rais amefanya utafiti na uchunguzi na kugundua vyuo vya Mzumbe na Chuo kikuu cha Dar ada zake hazizidi million mbili na hivyo achukue hela akalipe ada ili aendelee na masomo.

Hata hivyo Balozi Dkt Emmanueli Nchimbi amesikitika na kuumia sana kukosa mazishi ya kiongozi huyo anayekumbukwa kwa kuanzisha Taasisi mbalimbali hapa Nchini ambazo zinaendelea kufanya vyema sana.taasisi hizo ni kama vile TRA na zingine nyingi sana.

Anasema sababu ya kushindwa kuhudhuria ni kwa kuwa wakati huo kulikuwa na ugonjwa wa Corona ,ambapo viwanja vilikuwa vimefungwa na hivyo akashindwa kusafiri kuja Nchini kushiriki Mazishi,anasema kuwa ndio maana alipofika tu nchini alikwenda moja kwa moja kwa Mama Anna Mkapa Kumpa pole. Na kwamba leo anayo furaha kutembelea mahali alipo lala Hayati Benjamini Mkapa.

Baada ya kusikia maneno hayo Mimi Mwashambwa nimeona kuwa Inaonyesha Hayati Mzee Benjamin Mkapa alikuwa na moyo mzuri .maana nakumbuka kama sijakosea hata Mheshimiwa Ridhiwani Kikwete amewahi kusema hadharani kuwa alilipiwa ada na Hayati Mkapa.

Rai yangu ni kuwaomba viongozi na wote wenye uwezo na nafasi ya kifedha kuweza kusaidia wenye uhitaji na wasio na uwezo. Siyo tu kwa wale wanaowafahamu bali hata kwa wale ambao hawawafahamu lakini wamewaona kuwa wana shida na uhitaji.

Mwisho naendelea kuwakumbusha kwa maneno haya kutoka kwenye Biblia ndugu zangu. Kwa kila jambo na majira yake na wakati kwa kusudi maalumu chini ya mbingu.

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.View attachment 3055105

Kawaida wa UVCCM ana Masters??
 
Back
Top Bottom