Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Rest in Peace Jimbo la Kigamboni sasa lipo wazi kabla hata ya February kufika
Yes sure, you can't hate death, because it is the only way to attain Eternal life.If you hate death then logically you hate God.
Sasa sisi tufanyeje?Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile 1969-2024
Spika wa Bunge Mhe. Dkt. Tulia Ackson (Mb) anasikitika kutangaza kifo cha Mbunge wa Kigamboni, Mheshimiwa Dkt. Faustine Ndugulile kilichotokea usiku wa kuamkia leo tarehe 27 Novemba, 2024 nchini India alipokuwa akipatiwa matibabu.
"Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha Mbunge wa Kigamboni na Mkurugenzi Mteule wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Kanda ya Afrika, Mheshimiwa Dkt. Faustine Ndugulile. Kwa niaba ya Wabunge natoa pole kwa familia, wakazi wa Kigamboni na Watanzania wote. Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi", amesema.
Ofisi ya Bunge kwa kushirikiana na familia inaendelea kuratibu shughuli za mazishi na taarifa zaidi zitaendelela kutolewa.
BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA, APUMZIKE KWA AMANI.
Imetolewa na: Kitengo cha Mawasiliano na Elimu kwa Umma,
Ofisi ya Bunge,
DODOMA.
27 Novemba, 2024
View attachment 3162859
Huu ni Msiba Mkubwa sana hasa kwa Wanachama wa JamiiForums kwa kumpoteza Mwenzao Dr Faustine Ndugulile.
View attachment 3162839
Hivi karibuni, Dk Faustine Ndugulile Jumanne ya Agosti 27, 2024 alishinda nafasi ya Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Ukanda wa Afrika na alipaswa kuanza majukumu hayo mapya Februari 2025.
View attachment 3162854
View attachment 3162855
View attachment 3162860
Faustine Engelbert Ndugulile, alizaliwa 31 Machi 1969) ni mwanasiasa wa chama cha CCM nchini Tanzania na ni mbunge wa jimbo la Kigamboni tangu mwaka 2010.
Mnamo 1997 alipata shahada ya udaktari wa madawa katika Chuo kikuu cha Dar es Salaam na mwaka 2001 alipata shahada ya uzamili katika mikrobiolojia na chanjo katika chuo kikuu cha Dar es Salaam.
Dk Ndugulile ni nani?
Dk Ndugulile ni daktari mwenye uzoefu wa zaidi ya miaka 25 kwenye afya ya jamii ndani na nje ya nchi. Amewahi kuwa mwakilishi wa Bara la Afrika katika Taasisi ya kimataifa ya Ukimwi na mwanzilishi wa mtandao wa dunia kuhusu ugonjwa wa TB.
Pia amewahi kuwa Naibu Waziri wa Afya na Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari hapa nchini.
Machi 11, 2023, Dk Faustine Ndugulile aliteuliwa kuwa mjumbe wa kamati ya ushauri masuala ya afya ya Umoja wa Mabunge duniani (IPU). Kwa uteuzi huo unaofanywa na Rais wa umoja huo wa mabunge duniani, ulimfanya Dk Ndugulile kuwa sehemu ya wabunge 12 duniani wanaoishauri IPU kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu afya.
Uteuzi huo ulianza Februari 2023 ambao unadumu kwa miaka minne.
October 24, 2023 Dk Ndugulile akachaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa kamati ya ushauri ya masuala ya afya ya Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) katika uchaguzi uliofanyika Jijini Luanda nchini Angola.
Prove it .If you hate death then logically you hate God.
Hata hawa wasiojulikana wanapotea sana tu sema ndio hvyo haitangazwiWatu Smart wanapotea tuba baki na Wasiojulikana.
R.I.P Classmate
Dahhh. Tulisikia tetesi nyingi kuwa Bashite analitaka Jimbo lako 2025🤔
Asante mkuuDah! Poleni sana wafiwa kwa kumpoteza mpendwa wenu.
Katika mema yake alishawahi kuku kumbuka japo kwa chupa ya mvinyo??ndivyo Tena !
R.ip,back benja mwezangu
Hawezi kupata Jimbo bashite kichwa maji kileDahhh. Tulisikia tetesi nyingi kuwa Bashite analitaka Jimbo lako 2025🤔
Exactly.If you hate death then logically you hate God.
Kumbe alipinga ishu za covid?Mkuu wacha hizi.. unless unamjua vizur..
Alipotolewa kwa issue ya Barakoa na msimamo wake kuhusu Covid kwani alirudishwa tena?