TANZIA Dkt. Faustine Ndugulile, aliyekuwa Mbunge wa Kigamboni afariki Dunia

TANZIA Dkt. Faustine Ndugulile, aliyekuwa Mbunge wa Kigamboni afariki Dunia

Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile 1969-2024

Spika wa Bunge Mhe. Dkt. Tulia Ackson (Mb) anasikitika kutangaza kifo cha Mbunge wa Kigamboni, Mheshimiwa Dkt. Faustine Ndugulile kilichotokea usiku wa kuamkia leo tarehe 27 Novemba, 2024 nchini India alipokuwa akipatiwa matibabu.

"Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha Mbunge wa Kigamboni na Mkurugenzi Mteule wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Kanda ya Afrika, Mheshimiwa Dkt. Faustine Ndugulile. Kwa niaba ya Wabunge natoa pole kwa familia, wakazi wa Kigamboni na Watanzania wote. Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi", amesema.

Ofisi ya Bunge kwa kushirikiana na familia inaendelea kuratibu shughuli za mazishi na taarifa zaidi zitaendelela kutolewa.

BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA, APUMZIKE KWA AMANI.

Imetolewa na: Kitengo cha Mawasiliano na Elimu kwa Umma,
Ofisi ya Bunge,
DODOMA.
27 Novemba, 2024


View attachment 3162859

Huu ni Msiba Mkubwa sana hasa kwa Wanachama wa JamiiForums kwa kumpoteza Mwenzao Dr Faustine Ndugulile.
View attachment 3162839
Hivi karibuni, Dk Faustine Ndugulile Jumanne ya Agosti 27, 2024 alishinda nafasi ya Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Ukanda wa Afrika na alipaswa kuanza majukumu hayo mapya Februari 2025.
View attachment 3162854
View attachment 3162855
View attachment 3162860
Faustine Engelbert Ndugulile, alizaliwa 31 Machi 1969) ni mwanasiasa wa chama cha CCM nchini Tanzania na ni mbunge wa jimbo la Kigamboni tangu mwaka 2010.

Mnamo 1997 alipata shahada ya udaktari wa madawa katika Chuo kikuu cha Dar es Salaam na mwaka 2001 alipata shahada ya uzamili katika mikrobiolojia na chanjo katika chuo kikuu cha Dar es Salaam.

Dk Ndugulile ni nani?
DK.FAUSTINE NDUGULILEA lizaliwa March 1969 Mbulu mkoani Manyara,
Akapata elimu ya msingi na ya Sekondari nchini Zimbabwe na kisha kidato cha Tano na Sita katika shule ya Tambaza jijini Dar es Salaam.

Mwaka 1997 alipata shahada ya udaktari wa madawa katika chuo kikuu Cha Dar es salaam na mwaka 2001 alipata shahada ya uzamili ya mikrobiolojia na chanjo katika chuo kikuu Cha Dar es salaam.

Mtanzania huyu ni mwanachama wa chama cha Mapunduzi( CCM ) nchini Tanzania na ni mbunge wa jimbo la kigamboni tangu mwaka 2010.

Taaluma na kazi

Dk Ndugulile ni Daktari Tiba na ana Shahada ya Uzamili ya Tiba katika Tiba Mikrobiolojia na Kinga kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Shahada ya Uzamili ya Afya ya Umma (MPH) kutoka Chuo Kikuu cha Western Cape, na Shahada ya Kwanza ya Sheria (LL.B) kutoka Chuo Kikuu Huria cha Tanzania.

Pia aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Afya ya Bunge la Tanzania, Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Mabunge ya Kimataifa (IPU) Advisory Group Health na mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Mtandao wa Kamati za Afya za Bunge la Afrika (NEAPACOH).

Dk. Ndugulile aliwahi kuwa naibu waziri wa Afya wa Tanzania kati ya 2017-2020, pia aliwahi kuwa Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari 2020-2021.

Pia amefanya kazi kama mkurugenzi katika Wizara ya Afya Tanzania anayeshughulikia huduma za uchunguzi na pia meneja wa programu mwanzilishi wa Huduma ya Kitaifa ya Usambazaji Damu mwaka 2006.
Kati ya 2007-2010, aliwahi kuwa Mshauri Mkazi wa Vituo vya Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa (CDC) nchini Afrika Kusini akitoa msaada wa kiufundi kwa nchi nyingine nyingi kama vile Angola, Msumbiji, Tanzania na Rwanda.
Hapa Tanzania ukiwa smart sana kiakili, hama nchi ukazitumie kwingine au fanya biashara kimya kimya. Don't expose your talents.
 
Sumu inayopatikana kwenye chuchu za wanawake inajulikana kama "siyuan" katika baadhi ya tamaduni. Hii ni sumu ambayo inaweza kuathiri mtu ikiwa ataingiliana kimwili na mwanamke anayekumbwa nayo. Ikiwa mtu atanyonya chuchu hizo, sumu hiyo inaweza kuingia mwilini mwake na kusababisha madhara makubwa.

Kwa ujumla, sumu hii inachukuliwa kuwa hatari, na athari zake zinaweza kujumuisha matatizo makubwa ya kiafya. Dalili zinaweza kujumuisha maumivu makali ya tumbo, kichefuchefu, na hata matatizo ya mfumo wa neva. Wakati mwingine, sumu hii inaweza kuchukua muda fulani kuathiri mwili, na muda huu unaweza kutofautiana kulingana na kiasi kilichotumiwa na mwili wa mtu mwenyewe.

Ili kujikinga na sumu hii, ni muhimu kufahamu na kuelewa vyanzo vyake, na pia kuzingatia usalama katika mahusiano ya kimwili. Ikiwa unafikiri umepata athari kutokana na sumu hii, ni vyema kutafuta msaada wa kitaalamu haraka.

Ni muhimu pia kuzingatia kwamba habari nyingi kuhusu sumu hii zinategemea tamaduni na imani za sehemu husika, na hivyo ni muhimu kufanya utafiti zaidi ili kupata taarifa sahihi. Katika hali yoyote, usalama na afya ni kipaumbele, na ni vyema kuwa makini katika mahusiano ya kimwili.
Ww jamaa
 
Katika Qur'an:

Surah Al-A'raf (7:34): "Kila ummah (jamii) ina muda wake. Na wakati wake ukifika, hawawezi kucheleweshwa wala kuharakishwa hata kidogo." Hii inathibitisha kwamba kila nafsi ina muda maalum wa kuishi, na kifo hakijali mipango yetu.

Surah Al-Ankabut (29:57): "Kila nafsi itapata mauti. Kisha mtarejeshwa kwa Mola wenu." Aya hii inatufundisha kwamba kifo ni hakika, na hatuwezi kuepuka wala kuchelewesha wakati wake.


Katika Hadithi:

Mtume Muhammad (S.A.W) alisema: “Mchana na usiku ni wake Allah, na kila kilichomo ndani ya dunia na mbingu ni chini ya idhini yake. Kifo kitakuja kwa kila nafsi katika wakati wake, na hakuna anayeweza kuzuia." (Sahih Muslim) Hadithi hii inasisitiza kwamba hakuna anayeweza kupanga kifo au kujua wakati wake, kwani ni jambo linalosimamiwa na Allah pekee.


Ujumbe:

Mafundisho haya yanatufundisha kuwa, ingawa tunafanya mipango na juhudi za maisha yetu duniani, hatufai kuwa na dhana kwamba tutaishi milele. Kifo kitakuja kwa wakati wake, na tunapaswa kuwa tayari kwa ajili yake kwa kufanya matendo mema, kuishi kwa uadilifu, na kumtegemea Allah katika kila hali.
 
Huyu mheshimiwa yawezekana alifariki siku kadhaa huko nyuma, ila kwa mambo ya siasa wameamua kutuchanganya juu kwa juu na jambo la leo.

Kwamba wakifanya yao akili za watanzania ziwe kwa marehemu.
 
Back
Top Bottom