Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 5,352
- 15,876
Ahadi hiyo imetolewa leo Aprili 25, 2026 na Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais -TAMISEMI anayeshughulikia Elimu, Dkt Festo Dugange, wakati wa mahafali ya 21 ya kidato cha sita yaliyofanyika shuleni hapo wilayani Longido.
Dkt. Dugange amesema Serikali imepokea kwa uzito mkubwa changamoto hiyo na imejipanga kuboresha mazingira ya wanafunzi.
“Serikali imewasikia. Tumejipanga kutoa zaidi ya Shilingi Milioni 700 kwa ajili ya ujenzi wa bwalo jipya litakalokidhi mahitaji ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari Longido,” amefafanua.
Naye Mkuu wa Shule, Mwalimu Justine Swai, amesema walimu wamejipanga kikamilifu kuhakikisha wanafunzi wanafanya vizuri kitaaluma kwakuwa wamewaandaa vyema na wana imani kuwa watafanya vizuri.