Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 5,352
- 15,876
Serikali imesema huduma za afya ya akili zimeshajumuishwa kwenye vifurushi vya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), na hivyo wananchi wanaonufaika na bima wanaweza kupata matibabu hayo kwa mujibu wa mwongozo wa matibabu uliopo.
Akijibu swali la Mbunge wa Iringa Mjini, Mhe. Jesca Msambatavangu, Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel amesema kuwa, huduma za afya ya akili, ushauri nasaha, pamoja na huduma za kibingwa kama vile utengamao, zote zimetajwa kama huduma muhimu kwenye Mwongozo wa Matibabu (Standard Treatment Guideline – STG) na zinagharamiwa na NHIF.
“Huduma hizi zinalipiwa kwa kuzingatia aina ya dawa na ngazi ya kituo cha huduma, kwa mujibu wa mwongozo wa matibabu wa Taifa,” amefafanua Naibu Waziri Dkt. Mollel.
Serikali imeendelea kuhakikisha kuwa huduma za afya ya akili zinapewa uzito sawa na huduma nyingine za msingi, na kuimarisha upatikanaji wake kupitia mifumo ya bima ya afya kwa wote.
=======================
Serikali iko mbioni kukamilisha mchakato wa kuanzisha baraza la afya ya akili na kwa sasa wanakamilisha vitu vichache.
Naibu Waziri wa Afya, Dk Godwin Mollel ametoa kauli hiyo leo Jumatano Mei 7, 2025 ambapo amesema awali walikuwa na ahadi ya kuanzisha baraza hilo Mei mwaka huu, lakini kuna mambo hayajawekwa sawa.
Dk Mollel amesema hayo alipokuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Iringa Mjini, Jesca Msambatavangu ambaye ameuliza kuhusu ahadi ya Serikali ya kuanzisha baraza hilo ifikapo Mei mwaka huu imefikia wapi.
Katika swali la Msingi Msambatavangu ameuliza lini NHIF itajumuisha huduma za afya ya akili kwenye vifurushi vya bima ya afya.
Dk Mollel amesema Serikali inatambua umuhimu wa kuwepo kwa baraza hilo ambalo litasaidia katika masuala mazima ya Afya ya Akili.
Amesema huduma za matibabu ya afya ya akili, ushauri nasaha, na huduma nyingine za kibingwa ikiwemo huduma za utengamao, ni baadhi ya zilizoorodheshwa kama muhimu za afya kwenye mwongozo wa matibabu (Standard Treatment Guideline – STG).
Pia soma ~ Huduma ya Saikolojia ipatikane kwenye Bima ya NHIF, kuna watu wengi wana changamoto ya Afya ya Akili