Dkt. Gwajima: Kumsomesha binti ili uje umuoe ni ukatili kijinsia

Dkt. Gwajima: Kumsomesha binti ili uje umuoe ni ukatili kijinsia

Si nasikiaga Huwa anawajivu watu mitandaoni Kwa bahati mbaya Mimi sina Facebook,Twitter (x), TikTok, Instagram kwenye simu nna Telegram pamoja na jamii forum peke yake. Kwahiyo akipata muda na huku aje tumsalimie na kumuuliza maswali.
Ningependa afanye hvy.
Hata humu anajibu, lakini akiona maswali ni magumu huwa anatoka nduki, akiona maswali ni marahisi basi atajitahidi kuyajibu.
 
Na ikibainika kuna mwanaume anamsomesha binti ikiwezekana apigwe mvua 30 ndio hao hawahudhurii kwenye vikao halafu wanakuja kutuabisha wanaume, bora hata Mr.Kweka tunaweza kumtetea, huyo wakili na hao wengine wapigwe mvua tu
 
“Hivi kuna haja gani ya kumsomesha mtoto wa mtu wakati wazazi wake baba na mama yake wapo? Wewe unajiingizaje kwenye hiyo shughuli? Ni mkeo?

Tukiichukua hii kauli tukasema tuishi nayo na iwe applied kwenye jamii nadhani itaenda kuwa na madhara zaidi kwa Dada zetu.

Kwasababu kwenye dating siku hizi wanaume tunapewa majukumu ya wazazi.

So kama mnataka kuwe na fairness basi angalieni na maeneo mengine ambayo Mwanaume anagharamika na kisha mpime, je hayo yalikuwa ni majukumu yake kama mwenza au yalikuwa ni majukumu ya wazazi wake.
 
Tatizo huwa linakuja pale aliyesomeshwa anatoa majibu ya kumkera msomeshaji.mfano anakuambia kwa sasa huna hadhi ya kunioa.Yaani uniambia maneno ya hivyo hata kama sikutarajia kukufanyia jambo baya lazima itabidi nikaombe kibali cha kumiliki bomu la nyukilia ili kuja kumwadabisha mwenye maneno ya kukera.
 
Wataacha ndara.
 
Mweshumiwa upo sahihi wanaofanya hivyo wengi wao ni madomo zege piga utosini masimp hao
 
Tukiichukua hii kauli tukasema tuishi nayo na iwe applied kwenye jamii nadhani itaenda kuwa na madhara zaidi kwa Dada zetu.

Kwasababu kwenye dating siku hizi wanaume tunapewa majukumu ya wazazi.

So kama mnataka kuwe na fairness basi angalieni na maeneo mengine ambayo Mwanaume anagharamika na kisha mpime, je hayo yalikuwa ni majukumu yake kama mwenza au yalikuwa ni majukumu ya wazazi wake.
hahahaha, una hoja
 
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu, Dkt. Dorothy Gwajima amesema si sahihi kwa wanaume kuwasomesha mabinti kwa kigezo cha kuja kuwaoa watakapokuwa wakubwa.

Dkt. Gwajima alitoa kauli hiyo baada ya kuwepo kwa visa vingi vya mauaji, vingine vikidai kuwa ni wivu wa mapenzi unaosababishwa na mwanamke kumsaliti mwanaume baada ya kumsomesha.

Akizungumza kwenye kipindi cha Morning Trumpet kinachorushwa na kituo cha runinga cha Azam jana, Dkt. Gwajima alisema hata kama wazazi hawana uwezo wa kumsomesha binti, mwanaume hutakiwi kumsomesha ili uje kumuoa.

Alisema serikali imeweka taasisi za kuwasaidia kuwasomesha mabinti ambao wazazi au walezi hawana uwezo wa kuwasomesha, hivyo hakuna ulazima wa mwanaume kufanya hivyo.

“Hivi kuna haja gani ya kumsomesha mtoto wa mtu wakati wazazi wake baba na mama yake wapo? Wewe unajiingizaje kwenye hiyo shughuli? Ni mkeo?

“Yaani huyu unamwita binti, yupo kwa wazazi wao, wewe tu unaingia katikati lazima ujiulize,” alisema.

Aliongeza: “Nilikuwa hata kama umemsomesha ni ukatili. na kesi moja, eti mtu kalipa ng’ombe mahari Morogoro pale, halafu binti akaja kufika chuo kikuu, mtoto sijui yupo sekondari, ‘form one’ (kidato cha kwanza), sijui yupo ‘primary’ (shule ya msingi)…! Yeye mwanaume kashaanza uwekezaji, jamani!”

Alisema matatizo mengi nchini huanza kumpata binti pale anapokuwa ameshamaliza shule na kujipambanua kihisia kwenye mapenzi kwa mtu anaemhitaji.

Alisisitiza kwamba hawashauri wanaume kuwekeza kwa binti ambaye bado ana umri mdogo, kwa sababu bado binti huyo hajaamua kuchagua mwanaume wa kumpenda na akili yake bado haijawa na uamuzi mzuri.

Kwani huyo Waziri yeye mwenyewe hapo amefikaje? Anataka kufunga dirisha alilotumia kuingia ndani ili wenzake wasilitumie?
Ingawa yeye hakusomeshwa, ila michongo yote ya ajira hadi teuzi imefanywa na mafundi mitambo Studio.
By the way, anaweza akawa na point hapo kwenye umri mdogo, ila angekuwa soecific, umri mdogo ni upi, maana kusema sekindari ni umri mdogo si kweli, kuna WT na mazaga kibao na wanaoma watu wazima kabisa
 
Tatizo huwa linakuja pale aliyesomeshwa anatoa majibu ya kumkera msomeshaji.mfano anakuambia kwa sasa huna hadhi ya kunioa.Yaani uniambia maneno ya hivyo hata kama sikutarajia kukufanyia jambo baya lazima itabidi nikaombe kibali cha kumiliki bomu la nyukilia ili kuja kumwadabisha mwenye maneno ya kukera.
Ndio maana mnaambiwa msisomeshe hilo ni jukumu la mzazi wake
 
Back
Top Bottom