DogoWaNjombe
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 3,284
- 7,708
Video: Wasafi TV
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia kwa katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi, Dkt. Habiba Hassan Omar imesema miradi ya flyovers, daraja la Uzi pamoja barabara ya Paje Kitogani itarahisha shughuli za kijamii na kufungua fursa mpya za uchumi Zanzibar
Dkt Habiba ameeleza hayo wakati akifanya mahojiano maalum na Wasafi Media ilipofika ofisini kwake kutaka kujua tija itakayopatikana wakati wa kukamilika miradi hiyo
Dkt Habiba amesema mradi wa Flyover namba 1 katika eneo la Mwanakwerekwe pamoja na flyover namba 2 katika eneo la Amani unaendelea kwa hatua nzuri ambao ujenzi wake utagharimu Dola za Marekani Bilioni 18 na kuondosha usumbufu wa magari mara baada ya kukamilika
Akizungumzia kuhusiana na ujenzi wa daraja la Uzi Ng’ambwa amesema daraja hilo lenye urefu wa kilomita 2.2 ikiwa na upana wa mita 14 pamoja na barabara za kuunganisha vijiji vya Unguja Ukuu utakaojumuisha kilomita 7.6 ambao utagharami Dola za Marekani Milioni 14 huku akisema kuwa hatua hiyo ni sehemu ya kufuta kilio cha wananchi wa eneo hilo kwa zaidi ya miaka 40
Amesema pamoja na hatua hiyo pia serikali inaendeleza na ujenzi wa barabara ya Paje - kitogani yenye urefu wa kilomita 13 utakaogharimu dola za Marekani Milioni 18 lengo ikiwa ni kurahisisha huduma bora za Miundombinu ya Barabara
Amesema miradi yote hiyo inatekelezwa na Kampuni ya CCECC ambapo inatajwa baada ya kukamilika kwake Mwezi Oktoba mwaka huu itafungua fursa za Biashara, kilimo uchumi na uwekezaji kwa wananchi wa Zanzibar hasa kwenye maeneo husika