Dkt Mwakyembe na viongozi wengine wakubwa Serikalini tafadhali zungumzie mambo yenye tija katika Taifa letu ikiwemo ajira, elimu, miundombinu nakadhalika.
Swala la ushoga ni jambo la kipuuzi na halifai hata kidogo kuzungumzia. Swala hilo linahusiana na malezi kwahiyo wazazi na walezi wanapaswa kubeba hili jukumu. Kiongozi mkubwa serikalini unapozungumzia ni sawa na kushusha hadhi yako kwasababu ni swala linalohusiana na makalio leo hii tujadili makalio tutakuwa watu wa hovyo.
Wananchi wanataka kufahamu kuwa ni lini watapata ajira, ni lini gharama za maisha zitashuka, ni lini kodi itakuwa rafiki kwa wananchi na mengineyo mengi.