Dkt. Hezron Lwaitama anaandika

Lwaitama ni mpuuzi. Hata kama mimi ningekuwa Rais siwezi kwenda msiba wa mtu anayenitukana mitandaoni. Huo msiba unamhusu Maria kwa 100%. Kila mtu abebe msalaba wake. Pia msiba ni jambo la kifamilia zaidi.
Kwahiyo marehemu alikuwa anamtukana au vipi
 
Lwaitama ni mpuuzi. Hata kama mimi ningekuwa Rais siwezi kwenda msiba wa mtu anayenitukana mitandaoni. Huo msiba unamhusu Maria kwa 100%. Kila mtu abebe msalaba wake. Pia msiba ni jambo la kifamilia zaidi.
Marehemu Philemon Sarungi na Maria ni watu wawili tofauti.
Kila mmoja anatakiwa ahukumiwe kwa matendo yake mwenyewe.
 
Sasa kwanini unafikiri watu wanataka kumpa rais madaraka makubwa zaidi kwa kuhudhuria misiba? Halazimishwi ila ni mategemeo ya watu atoe salamu au kuhudhuria msiba wa mstaafu kama huyu.
kama unajua hayo ma beef sawa ila mategemeo ya watu hayakwepeki
Msiba ni jambo binafsi la familia.

Huu ni msiba wa familia ya Sarungi, licha ya kwamba Prof. Philemon Sarungi alikuwa mtumishi wa umma.

Wewe kama si mtu wa familia huna haki ya kutaka msiba wa familia ya watu uweje.

Unaweza kulazimisha rais atoe salamu za rambirambi kwa familia wakati marehemu kaacha wosia rais asihusike kabisa na msiba huo, na rais kashaambiwa, ndiyo maana hakutoa hata salamu za rambirambi, na wewe unapiga kelele kwa kutojua hizo habari, kwa sababu si sehemu ya familia.

Waacheni watu wamzike baba yao wanavyotaka.

Msiweke siasa kwenye misiba ya watu.
 
Wapumbavu kupitiliza
 
Angekuwa kajambakanani kama mimi na wewe, sawa. Public figure hiyo ndiyo maana hata taasisi za serikali zimetoa pole na baadhi ya viongozi kuhudhuria mazishi.
 
Angekuwa kajambakanani kama mimi na wewe, sawa. Public figure hiyo ndiyo maana hata taasisi za serikali zimetoa pole na baadhi ya viongozi kuhudhuria mazishi.
Hujaelewa somo bado.

Msiba ni wa familia ya Sarungi.

Profesa Philemon Sarungi kuwa public figure haiondoi ukweli kuwa msiba ni wa familia ya Sarungi.

Hujui familia ya Sarungi imetaka msiba wao uendeje.

Huna haki ya kusema msiba wa familia ya Sarungi uendeje.

Familia ya Sarungi ndiyo ina haki hiyo.

Jua sehemu yako iko wapi.

Ukipata msiba wa familia yako na wewe utapata haki ya kusema msiba wa familia yako uendeje.
 
Hili jawabu πŸ‘† πŸ‘† limekaa kitaalam zaidi
 
Msiba ni jambo la kijamii
Hata kwa hoja ya "msiba ni jambo la jamii" kuna muktadha wa mambo fulani ya msiba kuachiwa familia.

Msiba ni jambo la jamii kwa maana ya kwamba jamii ina jukumu la kui support familia katika msiba, ku support mambo ambayo familia inataka katika msiba. Si jukumu la jamii kuipangia familia msiba uende vipi.

Si jukumu la jamii kutaka expectations za jamii zifikiwe katika msiba. Msiba si fashion show. Msiba si sehemu ya mashindano ya umaridadi na umaarufu. Msiba si sehemu ya mashindano ya nani anajulikana mpaka Ikulu na rais. Msiba unaongozwa na familia, jamii ina play a supporting role tu kwa familia.

Mfano, marehemu akiacha wosia azikwe wapi na vipi, na familia yake kusimamia hilo, hutakiwi kuja na kubadili hilo ukisema "msiba ni jambo la kijamii, jamii inapanga marehemu azikwe sehemu tofauti na alipotaka, kwa namna tofauti na aliyotaka".

Hapo utaona kuwa, hata kama ni kweli msiba ni jambo la kijamii, kuna muktadha wa mambo ambayo familia ya wafiwa inaongoza kupanga msiba uendeje.

Na hapo ndipo Watanzania wengi wanaohemuka humu wanaposhindwa kutenganisha wapi msiba ni wa jamii na wapi familia iachiwe kuomboleza inavyotaka, kwa amani.
 
Siku CHADEMA mkishika dola badilisheni katiba kuwe na kifungu kinachomlazimisha Rais kuhudhuria misiba. Vinginevyo ulichoandika ni upumbavu mtupu.
Aliyekwambia mimi ni mfuasi au mwanachama wa CHADEMA ni nani?πŸ€”
Mkikaa huko jalalani ndipo huwa mnaambiana kuwa kila anae wachallenge au kuwapinga huwa ni CHADEMA sio?πŸ€”

Huku ni kukosa akili na maarifa. Unasahau kuna raia tuna operate nje ya mfumo wa vyama vya siasa na hatuna mitazamo ya mashindano ya vyama wala hatuna ajenda za kusiasa tunadeal na uzalendo kwa taifa letu tu?

Acha huu utoto na upumbavu.
 
Angeenda au asingeenda, haongezi wala kupunguza chochote kile.

Trivial issue.
Kama ambavyo aliudhuria msiba wa mtu mdogo Bwana Mafuru kwa kuupa uzito na kupuuza msiba wa Waziri wa ulinzi Mstaafu Profesa Sarungi.
Samia kapuyanga kwenye hili la Sarungi!!
 
Asante sana umenena vyema.Siasa kwenye misiba siyo jambo jema kabisa. Mara nyingi familia inasahaulika inaishia protocol kwa watu wasiohusika kabisa na mashada wanaweka wao
 
Sasa pale wewe ulimsikia nani akisema anawakilisha serikali?maana ata Waziri wa Afya au Naibu wake hakuwepo!
Mbona juzi kati CDF katumwa na Rais kupeleka ubani kwa Mzanzibari aliyefia kule DRC na wala hana cheo chochote ni koplo tu.
Kwenye hili la Professor Sarungi Samia kapuyanga sana!!
 
Asante sana umenena vyema.Siasa kwenye misiba siyo jambo jema kabisa. Mara nyingi familia inasahaulika inaishia protocol kwa watu wasiohusika kabisa na mashada wanaweka wao
Professor Sarungi amewai kuwa Waziri wa ulinzi, kwaiyo pia JWTZ walipaswa kuhusika na mazishi yake.
Kwenye hili la Professor Sarungi Samia kapuyanga sana,msitetee!!
 
Asante sana umenena vyema.Siasa kwenye misiba siyo jambo jema kabisa. Mara nyingi familia inasahaulika inaishia protocol kwa watu wasiohusika kabisa na mashada wanaweka wao
Kuna binti mmoja alinisimulia jinsi alivyokasirika msiba wa baba yake ulivyotekwa na wanasiasa maarufu, wakaanza kutoa hotuba zao mpaka za kisiasa msibani kwao huyo binti.

Binti alichukia sana ila alishindwa kufanya kitu.
 
Professor Sarungi amewai kuwa Waziri wa ulinzi, kwaiyo pia JWTZ walipaswa kuhusika na mazishi yake.
Kwenye hili la Professor Sarungi Samia kapuyanga sana,msitetee!!
Mkuu,

Una uhakika Professor Sarungi alitaka Samia ahusike kwenye msiba wake?

Unajua mazungumzo ya ndani ya familia ya Sarungi kuhusu hili jambo?
 
Ipo siku wa Tz wataujuwa ukweli.. tuzidi kuliombea Taifa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…