Hata kwa hoja ya "msiba ni jambo la jamii" kuna muktadha wa mambo fulani ya msiba kuachiwa familia.
Msiba ni jambo la jamii kwa maana ya kwamba jamii ina jukumu la kui support familia katika msiba, ku support mambo ambayo familia inataka katika msiba. Si jukumu la jamii kuipangia familia msiba uende vipi.
Si jukumu la jamii kutaka expectations za jamii zifikiwe katika msiba. Msiba si fashion show. Msiba si sehemu ya mashindano ya umaridadi na umaarufu. Msiba si sehemu ya mashindano ya nani anajulikana mpaka Ikulu na rais. Msiba unaongozwa na familia, jamii ina play a supporting role tu kwa familia.
Mfano, marehemu akiacha wosia azikwe wapi na vipi, na familia yake kusimamia hilo, hutakiwi kuja na kubadili hilo ukisema "msiba ni jambo la kijamii, jamii inapanga marehemu azikwe sehemu tofauti na alipotaka, kwa namna tofauti na aliyotaka".
Hapo utaona kuwa, hata kama ni kweli msiba ni jambo la kijamii, kuna muktadha wa mambo ambayo familia ya wafiwa inaongoza kupanga msiba uendeje.
Na hapo ndipo Watanzania wengi wanaohemuka humu wanaposhindwa kutenganisha wapi msiba ni wa jamii na wapi familia iachiwe kuomboleza inavyotaka, kwa amani.