Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 53,857
- 121,995
Si wengi wanajua hata burials zinalindwa na the right to privacy ndio maana kuna families wanazika kwa private burialHivi hawa watu wanaolazimisha rais awepo msibani wanajua hata Profesa Philemon Sarungi mwenyewe alitaka azikwe vipi?
Wanajua familia yake inataka azikwe vipi?
Au watu wanashoboka tu kuipangia familia?
Stephen Wasira, Makamu Mwenyekiti wa CCM, kaenda msibani, kapewa maneno yake na mjane wa Profesa Sarungi, kaambiwa hamkuonekana Profesa alivyokuwa anaumwa hata siku moja, leo amefariki mmekuja kufuata nini hapa?
Wasira akatoka nduki.
Sasa wanaolazimisha rais awepo wanajuaje kuwa Profesa Sarungi alitaka rais awepo?
Au watu wanalazimisha wanavyotaka wao tu bila hata kuangalia familia inataka nini?
P