Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 78,790
- 128,275
Hakuna uraia wa Zanzibar wala uraia wa Tanganyika.Zanzibar wana katiba yao ambayo haiwatambui watu wa Tanganyika kama ndugu zao
Mwinyi sio mnzazbar ni mtanganyika wa mkuranga
Mtu wa Tanganyika haruhusiwi kumiliki ardhi zanzibar lakini wanzazibar wanaruhusiwa huku Tanganyika
Mnzazbar anaruhusiwa kugombea uongozi Sehemu yeyote ile Tanzania lakini sisi Tanganyika ni Tanganyika tu
Kuna uraia wa Tanzania tu.
Kwa hivyo, unaposema "Mtanganyika", hii dhana ni ya uzushi tu. Hakuna uraia wa "Mtanganyika".
Hakuna hata kabila la "Mtanganyika".
Haya. Tuseme kuna watu wa bara na Wazanzibari. Na Wazanzibari wabaguzi kweli, wanabagua watu wa bara.
Kama Wazanzibari wanabagua watu wa bara, na kina Mwinyi wameona sawa tu, wamelowea huko Zanzibar, wameoa huko, wameamua wazikwe huko, wewe tatizo lako nini?
Yani wewe leo unataka kusema unawapenda kina Mwinyi kuliko wanavyojipenda wenyewe?