Alwatan Mabruki
Senior Member
- Sep 20, 2020
- 132
- 116
SOMA HII KWA MAKINI KWANZAMiddle income country ??!! ---- before he became president a kilo of sugar cost at 1,800/= just after he became the price skyrocketed to 2,500/= to 3,500/= in some places, and he keeps blind eyes on the menace etc, without legal salary increase to public workers in his 5 dark torturous years.
FACT KUHUSU WATUMISHI NA MAGUFULI
Kwa kipindi Cha miaka mitano Rais Magufuli amewafanyia Nini watumishi wa Tanzania? Hili Ni swali ambalo huwa halijibiwi na kwa kutokuwa na taarifa Wapinzani wamekuwa wakipotosha baadhi ya Mambo.
1. Cha kwanza alichokifanya aliwaondoa kazini watumishi wote wa Umma waliokuwa na Vyeti fake Jumla yao ikiwa 15,508.
2. Jambo la Pili alifanya Uhakiki wa watumishi wa Umma na kugundulika kuwa Juma Watumishi hewa 19,708 walikuwa Ni hewa yaani analipwa mshahara mtu asiyekuwepo. Kwa kufanya hivyo alifanikiwa kuokoa shilingi bilioni 19. 8 kila Mwezi zilizokuwa zikipotea.
3. Jambo la tatu alilofanya kwa miaka mitano aliajiri Watumishi wapya 74,173. Kama nafasi za waalimu 13,000 zilizoombwa wataajiri mwaka huu kabla ya uchaguzi mkuu atafikisha Jumla ya watumishi 84,173 walioajiriwa kwenye awamu yake ya kwanza Kama Rais.
4. Jambo la nne lililofanyika Ni kwamba Jumla ya watumishi Waliopandishwa Vyeo katika kipindi Cha miaka mitano Hadi siku ya kulivunja Bunge walikuwa Jumla ya watumishi 306,917.
5. Jambo la tano muhimu lililofanyika kwenye awamu hii ya kwanza ya Rais Magufuli ni kulipa Madeni ya kimshahara na yasiyo ya kimshahara Jumla ya Bilioni 472.6.
6. Jambo la Sita na la muhimu Sana Ni kuwa alishusha Makato ya PAYE toka asilimia 11 Hadi asilimia 9 kwa wafanyakazi wote wa Serikali.
Watumishi wa Serikali wanaelewa ninachokiongea hapa. Wale wa story za vijiweni Karibu kwa kupinga.