Kabende Msakila
JF-Expert Member
- Oct 7, 2020
- 1,809
- 1,692
Waheshimiwa:-
Dkt. John Pombe Magufuli
Adv Tundu Antipas Lissu
Maalim Seif Sharif Hamadi
Dkt. Hessein Ally Mwinyi, na
Wengine - Salaam za 28/10/2020!!!
Kwa niaba ya wapenda amani, haki, usawa, maendeleo na maridhiano nimeandika uzi huu kwa ajili ya kuwapongeza sana sana kwa kushiriki kampeni za mwaka 2020.
Kiukweli mmeandika historia isiyoweza kufutika katika vichwa vya watanzania na wapenda upendo duniani. Haikuwa kazi nyepesi kuzunguka nchi nzima na kumaliza wote mkiwa salimini ingawa misukosuko kadhaa ilijitokeza kwa baadhi ya makamu na wenyeviti wenu.
Maombezi kwenu:-
Kwa imani ndogo niliyonayo nawaombea sana asubuhi ya leo kukipambazuka mshiriki vema shughuli ya upigaji kura - nawaombea sana kupokea matokeo yatokanayo na kazi ya wapigakura wenu (watanzania). Nawaombea sana kukubaliana na matokeo kwa kuwa jukumu lenu mmemaliza na lililobaki ni jukumu msiloweza kulipangua - utashi wa wapigakura. Hivyo, kila mmoja wenu ajiandae kupokea kadri alivyowekeza kwa wananchi.
Ushauri yakinifu:-
Nikiwa miongoni mwa watanzania wengi wapenda maendeleo na mshikamano nitafurahi sana ikiwa tofauti zenu za kikampeni zikiisha leo - tofauti za kivyama zikiisha leo - habari ya mimi ikiisha leo ili kuanzia matokeo kutangazwa wote muimbe Tanzania Tanzania Tanzania - atakayeibuka mshindi aone kuwa ipo haja ya kuongoza na wenzake ili kubalance mambo.
Mwisho:-
Watanzania tuko tayari kuwapa ushirikiano wakati mtakapoanza kutekeleza majukumu yenu.
Mungu ibariki Tanzania,
Mungu ibariki Afrika
Msakila M Kabende
Kigoma - Tanzania
28 Oktoba, 2020