JF members, and Tanzanians!
Dkt John Pombe Magufuli amefanya mengi mazuri kwa taifa letu la Tanzania - ni ngumu kutaja kwa jina kila alichofanya lakini kwa uchache - elimu, afya, barabara na vivuko, uwajibikaji, makusanyo na kodi, matumizi ya fedha za umma na kukomesha Ufisadi ni miongoni mwa vita aliyoshinda nchini.
Vita ambayo bado ni ngumu kutokana na ongezeko la idadi ya watu ni pamoja AJIRA kwa vijana, mkakati wa kuwainua WAKULIMA, habari na vyombo vya habari, uwiano mkubwa wa mishahara ya watumishi wa Umma, kukawizwa kwa pensheni za wastaafu, na Katiba ya Warioba.
SASA
Dkt John Pombe Magufuli akiridhia nimpokee kijiti cha urais baada ya muda wake kufikia mwisho kikatiba basi maeneo niliyotaja hapo juu nitayapa kipaumbele bila kusahau core "muungano wetu na kulinda maslahi ya watangulizi wangu ambao ni Dkt John Pombe Magufuli, Dkt Jakaya Mrisho Kikwete, Mzee Ally Hassan Mwinyi, na familia ya mwasisi wa taifa Mwl Nyerere".
Kwa kuwa kuisha kwa uchaguzi mmoja ndiyo mwanzo wa uchaguzi mwingine basi nasubiri kipenga kipulizwe ili nipokee kijiti hicho kwa mwaka 2025 - 2030.
Siwachoshi niwasilishe
Mungu ibariki Tanzania
Mungu mbariki Rais Magufuli!
Msakila M Kabende
Kigoma
11/01