Kabende Msakila
JF-Expert Member
- Oct 7, 2020
- 1,809
- 1,692
Wanabodi, Salaam.
Nimeona kupitia mitandao ya kijamii kuhusu utenguzi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya Igunga mkoani Tabora leo tarehe 28 Desemba, 2020.
Kwa ujumla iwapo Mkurugenzi huyo alikuwa na kasoro lazima atenguliwe kupisha wenye uwezo, ubunifu na wanaojali kuongeza mapato ya halmashauri, wanaoweza kutumia vizuri mapato yaliyokusanywa. Hata hivyo najiuliza na kuwauliza tu kutokana na utamaduni tuliozoezwa:-
(I). Siyo kawaida kutengua Mkurugenzi na kukaimisha nafasi hiyo - huenda ile bandika bandua imeisha kwa wenye sifa kukosekana?
(ii). Dkt John Pombe Magufuli huenda amefanya hivyo sababu yuko sikukuu za Christmas na mwaka mpya?
(iii). Athari za kukaimisha ni kubwa sababu aliyekaimishwa huwa hana hali ya kujiamini - maamuzi yake ya kutojiamini yanaweza kusababisha halmashauri kurudi nyuma kwa kasi.
Mapendekezo
Kama alivyotuzoeza ikitokea utenguzi basi na uteuzi ufanyike kwa kuwa najua kuna hazina kubwa ya wenye sifa i.e waliogombea ubunge uchaguzi mkuu, waliogombea ubunge kura za maoni, wakuu wa idara ktk sekretarieti za mikoa na halmashauri nk
Mwisho
Nimtakie afya njema yeye na wasaidizi wake lkn pia niwaombee mwaka mpya 2021 wenye fanaka.
Msakila M K
Kigoma