Kabende Msakila
JF-Expert Member
- Oct 7, 2020
- 1,809
- 1,692
Wanabodi, Salaam!
Kwanza nianze kwa kukupongezeni kwa uhai wenu ndani ya kundijamii hili - nafahamu kwamba pamoja na kuwa tumo watu wa itikadi tofauti za vyama vya siasa, dini tofauti, jinsia na makabila tofauti lkn bado tunatumia jukwaa hili kutoa ya akikini mwetu ili yasaidie kuijenga nchi yetu. Hongereni!
Pili nchi yetu imekuwa wakati mwingine ikipitia vipindi kadhaa vigumu hususan nyakati za uchaguzi mkuu - migogoro midogo kwa mikubwa imekuwa ikitokea miongoni mwa makundi ya wanasiasa na vyama vyao. Lkn ukomavu wa kidiplomasia walionao viongozi wetu ndiyo imekuwa kinga na msaada kwa taifa kutoingia kwenye machafuko na umwagaji damu.
Nasema haya kwa kuwa kitendo cha Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kufikia mwafaka unaotokana na mgogoro wa kiuchaguzi wa nyuma, wakati na baada ya tarehe 28 Oktoba kati ACT Wazalendo (Maalim Seif), na CCM (Dkt Magufuli na Dkt Mwinyi) cha kukubali kufanya kazi kama timu moja kinastahili pongezi nyingi sana na zawadi yenye kumbukumbu isiyofutika kwa viongozi hao.
Ndiyo sababu nashauri, napendekeza, na kuonelea kwamba viongozi hao watatu yaaani:-
(i) Dkt John Pombe Magufuli,
(ii) Dkt Hussein Mwinyi, na
(iii) Maalim Seif S Hamad - watunukiwe udaktari wa heshima kwa kukubali kumaliza mambo magumu na mazito kwa njia ya mazungumzo.
Nanyi CHADEMA, NCCR, CUF, nk jifunzeni maridhiano toka kwa wazee wetu hao. Wakati wa Mungu ukifika mtatawala - na kamwe tusisukumwe na hulka za Wabeligiji na vibaraka wengine ambao wana nia ovu kwa taifa letu
Msakila M Kabende
Bukoba
Kagera
06 Desemba, 2020.
************
Kitendo cha Maalim Seif Sharifu Hamad ukukubali wito wa Dkt John Pombe Magufuli na Dkt Hussein Mwinyi kuunda Serikali ya Umoja wa kitaifa ni cha kupigiwa mstari - hapo hata mabeberu yamevunjika moyo - hili hata Joe Biden USA hataliweza dhidi ya Donald Trump.
Heko JPM, HM, SSH!
Mungu ibariki Tanzania