beth
JF-Expert Member
- Aug 19, 2012
- 3,881
- 6,377
WAZIRI wa Nishati Dk Medard Kalemani ameagiza taasisi za umma ambazo zinadaiwa zaidi ya Sh bilioni 182 na Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) kukatiwa umeme.
Alisema hayo jana mjini hapa wakati akizungumza na wenyeviti wa bodi na wajumbe wa bodi za Tanesco, Wakala wa Umeme Vijijini (REA), Mamlaka ya Udhibiti wa Shughuli za Mkondo wa Juu wa Mafuta (PURA),Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) na Bodi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA)
Aliagiza Tanesco kwenda kukata umeme kwa wateja wasiolipa ikiwa ni Sh bilioni 186 ambazo ni taasisi za umma huku wateja wa kawaida wakidaiwa zaidi ya Sh bilioni 3.6.
“Kateni umeme na atakayekuja kulalamika anilalamikie mimi ,bodi ya Tanesco kakateni umeme, tunataka kupata fedha za kupeleka umeme ,lazima tuongeze mapato, nilishasema simuombi fedha Rais… hiki ni kikao kazi muhimu kwa ajili ya kuanza kazi pamoja, kwenda pamoja na kufika pamoja.'Kauli mbiu yetu kasi, ubunifu, usahihi',” alisema.
Waziri Kalemani alisema alianza kwa kukutana na watendaji wa Wizara na sasa anakutana na bodi.
“Sitaki kuona umeme unakatika hovyo. Sitarajii mgao wa umeme au umeme kukatika hovyo, kwenye kukatika umeme sitavumilia sisi ni injini ya kukuza viwanda, ukiona meneja hakufai kwenye eneo lako , umeme una katikatika fukuza , dosari ndogo ndogo kaziondoeni kipaumbele cha Tanesco kuzalisha umeme wa kutosha,” alisema.
Aliwataka pia kukamatwa kwa wezi wa umeme kwani bado wapo.
“Kigoma na Katavi tumeanza kupeleka gridi ya taifa kutoka Tabora umbali wa kilomita 364 nataka mradi huo ukamilike ndani ya miezi minne ili waondokane na umeme wa kutumia mafuta,” alisema na kusema Kigoma itaunganishwa na gridi ya taifa na tayari fidia imeshalipwa.
Alisema pia hataki kusikia lugha ya kuwaambia wateja nguzo hakuna na akisikia jambo hilo , meneja huyo atakuwa hatoshi na kuongeza kuwa maeneo wananchi wamelipia ĺakini hawajaunganishwa na umeme, mwananchi akiona anazungushwa zungushwa aende kwa mkuu wa wilaya na risiti zake hata ikibidi ikibidï uende hata polisi,” alisema.
Waziri Kalemani alisema Tanesco wamepewa Sh biĺioni moja za kusambaza umeme vijijini kwa nini wauze nguzo na kusema kuwa ni marufuku kumueleza mteja aje na transfoma kwani hiyo ni malï ya Tanesco.
Aĺiitaka kiĺa meneja atatue kero kwenye eneo ĺake kwani suala la kuunganisha wateja ndio sehemu ya mapato na pia alipiga marufuku bodi hizo kumpa zabuni mkandarasi mwenye bei ya juu na kuacha wa chini.
Alitoa maelekezo kwa Katibu Mkuu wa wizara hiyo kuwa masuala yote yanayohitaji muundo ikiwemo wale wanakaimu waweze kudhibitishwa inapobidi kwani hawawezi kuwa na watendaji ambao bado hawajiamini.
Naibu Waziri wa Nishati Sephen Byabyato aliomba ushirikiano ili waweze kufanya kazi ya kuwaletea wananchi maendeleo.