Hapa kwenye huu uzi kuna jambo dogo nimejifunza, wasiomtaka Mbowe hawajui maana ya demokrasia, simply wanalazimisha matamanio yao yawe uhalisia.
Mfano tukisema hapa tupige kura wanaomtaka Mbowe aendelee kuwa mwenyekiti Chadema, na wasiomtaka, ni obvious wanaomtaka aendelee kuwa mwenyekiti watashinda, lakini ajabu hao wasiomtaka hawawezi kuheshimu mawazo ya wenzao, ajabu zaidi hawa ndio wanajidai kuijua demokrasia!.
Uamuzi wa Mbowe kugombea uenyekiti ni wake binafsi, wajumbe ndio wenye maamuzi ya mwisho kama wanamtaka aendelee watampigia kura, kama hawamtaki watamnyima kura, nyie wachache msiomtaka Mbowe mnateseka kwa nini?
Fanyeni hivi, simply tafuteni mgombea wenu mtaemuona anaweza kumshinda Mbowe mkampigie kura kama mnaweza, isijekuwa hata kura zenyewe hamuwezi kupiga halafu mnataka mgombea mumtakae achaguliwe mwenyekiti wa Chadema.
Hata suala la kusema Mbowe kazidisha muda aondoke kwani nyie ndio katiba ya Chadema? au mnadhani kuna kuachiana madaraka kienyeji tu kwa sababu za kimahaba? au kwasababu ACT wamebadilisha uongozi, kwani ACT ndio kipimo kwa Chadema kujiamulia mambo yao?
Simply Kigwa kaongea ujinga, na wote mnaomuunga mkono ni wajinga kama yeye.