kwani demokrasia kwa tafsiri yako ni nini?
Demokrasia ni katiba ya nchi au chama ambayo inampa kiongozi wa chama au nchi akae madarakani kwa muda fulani uliyowekwa na chama au nchi husika.
Katiba ya Chadema iliyotungwa wakati wa uanzishaji wa chama ilikuwa ni ya mihula miwili tu ya miaka mitano mitano. Mwenyekiti wa chama aliechaguliwa kidemokrasia na chama aliruhusiwa kukaa madarakani kwa muda wa miaka mitano ya muhula wa kwanza, na endapo atahitaji kuendelea basi itabidi agombee tena na akishinda amalizie muhula wa pili.
Muongozo wa katiba hiyo ulifuatwa na viongozi wote waliotawala kabla ya Mbowe. Alianza mzee Mtei akatawala, mihula yake ilipoisha akatoka kwa mujibu wa katiba na kumpisha mgombea mungine aliegombea na kushinda uenyekiti (Bob Makani)
Marehemu Bob Makani nae akafuata katiba ya chama kwa kutawala mihula miwili kisha akaacha wagombea wengine wapambane, mshindi akawa Mbowe, Bob Makani akamkabidhi kijiti kwa mujibu wa katiba ya chama.
Mziki ukaja kwa Mbowe ambae hakutaka kutoka katika kiti, akaamua kubadilisha katiba ili aendelee kuwa anagombea miaka yote mpaka uzeeni. Na kwa mazingira yetu ya kiafrika ni vigumu sana mtu wa kawaida kushindana na kiongozi aliepo kwenye kiti, maana yeye ndo boss wa wapiga kura wote, na pia boss wa wahesabu kura wote.
So ni rahisi mno kuwadhibiti, kuwahonga au kuwatisha ili wampitishe. Nafikiri umeshasikia Lisu akilalamika juu ya rushwa inavyotembea katika chaguzi. Sasa kwa mantiki hiyo hata kama wanachama hawamtaki mwenyekiti yeye ataendelea kupita tu kwa sababu ana hela za kuwahonga.
kwani hawaruhusu watu wengine kugombea? mbowe huwa anapita bila kupingwa? nisaidie mkuu maana mimi nimezaliwa 2010
Kushindana na mtu aliebadilisha katiba ili miaka yote aendelee kutawala ni kazi bure. Yeye ndio kiongozi wa wapiga kura na wahesabu kura, hivyo uwezekano wa uchaguzi huo kuwa wa haki ni mdogo sana. Ni sawa na mpinzani ashindane na raisi katika uchaguzi. Uwezekano wa mpinzani huyo kushinda uchaguzi huo ni mdogo sana hata kama yeye atakuwa amepata kura nyingi kushinda raisi.
So mkuu usidanganyike na watu kuchukua fomu kushindana na Mbowe, ile ni geresha na hata hao wachukuaji fomu hujua kabisa kwamba hawatoweza kushinda kwa namna yoyote ile.