Dkt. Kigwangalla: Mo Dewji siyo rafiki yangu tena atabaki kuwa jamaa tu, hajasababisha nipoteze Uwaziri

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Aliyekuwa waziri wa maliasili na utalii Dkt. Kigwangalla amesema amefuta rasmi urafiki wake na mfanyabiashara maarufu Mo Dewji kwa sababu yeye (Kigwangalla) ni mtu wa principles.

Akizungumza na Salama Jabir wa Eatv Dkt. Kigwangalla amesema baada ya mzozo wa mkopo wa pikipiki Mo Dewji alimpigia simu zaidi ya mara tatu ili wakae chini wayamalize lakini alimkatalia kwa sababu ameshafuta urafiki na sasa watabaki kama jamaa tu kila mtu kivyake.

Dr Kigwangalla amesisitiza kuwa hajafutwa uwaziri kwa sababu ya malumbano yake na Mo Dewji bali muda wake wa kuhudumu kama waziri ulikwisha.

Kuhusu pikipiki Dr Kigwangalla amesema Mo Dewji alimnyima mkopo lakini akaamua kuzinunua kwa cash pale pale hivyo mjadala wa pikipiki ulishafungwa kiuhasibu na kibiashara.

Chanzo: EATV

Pia soma

Maendeleo hayana vyama!
 
CCM imejaa vichaa. Tangu lini maskini akamchukia tajiri?

Mwenye hela hanuniwi hata siku moja! Mo aache kuwapigia simu wasimamizi wake wa biashara ampigie huyu chizi!?

Kigwangala anatafuta kiki ya kutokea baada ya kukosa uwaziri.
 
Duu hatari sana bado tu anaendeleza mambo ya media
 
Ni jambo jema.
085e4335cfc0e3a3b34ee11a2dd7fdec.jpg
 
CCM imejaa vichaa. Tangu lini maskini akamchukia tajiri?

Mwenye hela hanuniwi hata siku moja! Mo aache kuwapigia simu wasimamizi wake wa biashara ampigie huyu chizi!?

Kigwangala anatafuta kiki ya kutokea baada ya kukosa uwaziri.
Maskini kumchukia Tajiri ni Principle ya Serikali ya Awanu ya tano...
 
Hawa wote wlifanya michezo ya kitoto sana.
HK kumhoji Mo kupitia social media ilhali ana namba yake na pia kuna vikao vya chama ni uzwazwa wa kiwango cha lami...hata kama angekua na nia njema kiasi gani...kila mtu angehisi ni hasira za kukosa mkopo wa pikipiki.

Kwa mfanya biashara mkubwa kama Mo dewj kumuweka hadharani tena mtandaoni mteja aliyetaka kumkopa...huu nao ni utoto..hakuna aliyetegemea kitu kama kile kutoka kwa mfanya biashara mkubwa Tanzania na Africa kiujumla.

Wangekua na busara hili suala wangeacha kuliongelea kwani hakuna awezaye kujisafisha zaidi kukumbusha watu upuuzi wao.
 
Nimekuelewa bwashee!
 
Back
Top Bottom