Dkt. Kigwangalla: Mo Dewji siyo rafiki yangu tena atabaki kuwa jamaa tu, hajasababisha nipoteze Uwaziri

Dkt. Kigwangalla: Mo Dewji siyo rafiki yangu tena atabaki kuwa jamaa tu, hajasababisha nipoteze Uwaziri

Kigwangala alikua anamuona MO rafiki MO anamuona hamisi chawa
 
Kigwangwala anaugua ugonjwa unaoitwa post cabinet selection mental disorder,sio mzima huyu
Si aliomba radhi?kwa kuwa kakosa uwaziri anafuta urafiki?vipi wana msimbazi tuchukue na hicho kiti??
Dawa yake ni kutulia nyumbani na kuangalia Tv mpaka Mungu atakapoamua
 
Huyu Waziri inakuwaga Kama akili yake siyo nzuri, kinachonishtuaga zaidi kwake ni yeye kushindwa kuandika hata sentence mbili za kiingereza kwa usahihi.
Ndiyo watu anaowapenda Magufuli sasa. Anataka watu wenye upeo ulio chini ya upeo wake, sasa fikiri mwenyewe ni watu wa aina gani!
 
Urafik kati ya tajiri wa pesa na mwenye power
 
Bila kuwa Mawaziri, kuna watu kama huyu Hamisi wangekuwa watu wa kawaida saana. Tusingewatofautisha na watendaji kata.

Heshima ile ya kisiasa imeondoka, ila bado haamini au labda hajui.
 
Huyu Waziri inakuwaga Kama akili yake siyo nzuri, kinachonishtuaga zaidi kwake ni yeye kushindwa kuandika hata sentence mbili za kiingereza kwa usahihi.
Jamaa mswahili tena bila shaka Ni mnyamwez itashangaza km atashindwa kuandika sentesi mbili Kwa kiswahili au kinyamwez lkn hicho kizungu tulijifunza kujibia mtihan tu ukishapata vyeti unabak nacho cha kuandikia barua tena kile cha kukarir ndio maana wasom wetu weng wanaungaunga tu.
 
Huyu si aliiba vyeti, sio jina lake hilo, very hopeless
 
Huyu Waziri inakuwaga Kama akili yake siyo nzuri, kinachonishtuaga zaidi kwake ni yeye kushindwa kuandika hata sentence mbili za kiingereza kwa usahihi.
Inawezekana ni kwasababu yy hatumii grammar editor kama wewe na wengine wengi
 
Hamis anazidi kuniharibia na hajui kama anaharibu
 
Aliyekuwa waziri wa maliasili na utalii Dkt. Kigwangalla amesema amefuta rasmi urafiki wake na mfanyabiashara maarufu Mo Dewji kwa sababu yeye (Kigwangalla) ni mtu wa principles.

Akizungumza na Salama Jabir wa Eatv Dkt. Kigwangalla amesema baada ya mzozo wa mkopo wa pikipiki Mo Dewji alimpigia simu zaidi ya mara tatu ili wakae chini wayamalize lakini alimkatalia kwa sababu ameshafuta urafiki na sasa watabaki kama jamaa tu kila mtu kivyake.

Dr Kigwangalla amesisitiza kuwa hajafutwa uwaziri kwa sababu ya malumbano yake na Mo Dewji bali muda wake wa kuhudumu kama waziri ulikwisha.

Kuhusu pikipiki Dr Kigwangalla amesema Mo Dewji alimnyima mkopo lakini akaamua kuzinunua kwa cash pale pale hivyo mjadala wa pikipiki ulishafungwa kiuhasibu na kibiashara.

Chanzo: EATV

Pia soma

Maendeleo hayana vyama!

Urafiki wa kujipendekeza tu. Waziri anayependa drama hivi angeingia kwenye bongo flava
 
Back
Top Bottom