Dkt. Kigwangalla: Mo Dewji siyo rafiki yangu tena atabaki kuwa jamaa tu, hajasababisha nipoteze Uwaziri

Dkt. Kigwangalla: Mo Dewji siyo rafiki yangu tena atabaki kuwa jamaa tu, hajasababisha nipoteze Uwaziri

Fikiria kama angefanikiwa kukopeshwa zile tukutuku......malipo yangekuwa ni " full sound" baada ya kitumbua cha uwaziri kuingia mchanga!
Ingembidi Mo asubiri kipindi cha uwaziri kikome ndio aulizie 'deni' lake, tena mbaya zaidi angepewa uwaziri wa michezo ndio wangekuwa 'wamemalizana' rasmi, Mo akiulizia 'deni' anapigwa fine kwa 'Mnyama' anajilipa mwenyewe!!
 
Hamisi anapenda ubishi na visasi kama Magufuli. Watu wa kanda ile muna shida gani? Mimi mtu wa ukanda wa Pwani nimeolea kule kanda ya Ziwa nazijua vizuri tabia za wakwe zangu na shemeji zangu.
 
Kigwangala hukutakiwa kwenda kwenye vyombo vya habari na kueleza hayo hapo sasa unaonekana una Nongwa
 
Aliyekuwa waziri wa maliasili na utalii Dkt. Kigwangalla amesema amefuta rasmi urafiki wake na mfanyabiashara maarufu Mo Dewji kwa sababu yeye (Kigwangalla) ni mtu wa principles.

Akizungumza na Salama Jabir wa Eatv Dkt. Kigwangalla amesema baada ya mzozo wa mkopo wa pikipiki Mo Dewji alimpigia simu zaidi ya mara tatu ili wakae chini wayamalize lakini alimkatalia kwa sababu ameshafuta urafiki na sasa watabaki kama jamaa tu kila mtu kivyake.

Dr Kigwangalla amesisitiza kuwa hajafutwa uwaziri kwa sababu ya malumbano yake na Mo Dewji bali muda wake wa kuhudumu kama waziri ulikwisha.

Kuhusu pikipiki Dr Kigwangalla amesema Mo Dewji alimnyima mkopo lakini akaamua kuzinunua kwa cash pale pale hivyo mjadala wa pikipiki ulishafungwa kiuhasibu na kibiashara.

Chanzo: EATV

Pia soma

Maendeleo hayana vyama!
Kweli maendeleo hayana vyama.
 
Bado ana frustrations tumpe wakati
Sidhani km ana tatizo kukosa uwaziri kwa sababu alijua kabisa si ajira ya kudumu.Na sii yy wa kwanza kupita apo wizarani.Ila jua tu ndugu yey alishachuma za kumtosha .ata mkimtukana,mkimbeza haisaidii.
 
Aliyekuwa waziri wa maliasili na utalii Dkt. Kigwangalla amesema amefuta rasmi urafiki wake na mfanyabiashara maarufu Mo Dewji kwa sababu yeye (Kigwangalla) ni mtu wa principles.

Akizungumza na Salama Jabir wa Eatv Dkt. Kigwangalla amesema baada ya mzozo wa mkopo wa pikipiki Mo Dewji alimpigia simu zaidi ya mara tatu ili wakae chini wayamalize lakini alimkatalia kwa sababu ameshafuta urafiki na sasa watabaki kama jamaa tu kila mtu kivyake.

Dr Kigwangalla amesisitiza kuwa hajafutwa uwaziri kwa sababu ya malumbano yake na Mo Dewji bali muda wake wa kuhudumu kama waziri ulikwisha.

Kuhusu pikipiki Dr Kigwangalla amesema Mo Dewji alimnyima mkopo lakini akaamua kuzinunua kwa cash pale pale hivyo mjadala wa pikipiki ulishafungwa kiuhasibu na kibiashara.

Chanzo: EATV

Pia soma

Maendeleo hayana vyama!
Kwa hiyo Kigs amemkoa mo? maana yake mo atajuta saana kukosa urafiki na Kigs?.labda kama ni urafiki wa kichawi au kinganga. otherwise Mo atakuwa amefurahi maana najua alikuwa anahitaji kupunguza marafiki wa ain ya kigs
 
Mwenye hela hanuniwi hajamuona Patel alivyo angwa & chomwa kwa heshima kubwa.

MO kasha kuwa next level saizi yake ni akina msukuma,
 
Back
Top Bottom