Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Dah umeua kabisa[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]Huyu mzee moja ya ahadi zake alizoshindwa kutimiza ni kuileta Real Madrid uwanjawa Taifa. Yaani kaenda mwenyewe tu kupiga picha Bernabéu
Jitoe kwenye unegativu Mkuu,ushauri uwa unatolewa baada ya kukosea....hizo picha kuwepo kwenye mtandao hazizuii MTU kupewa hushauri pale alipokosea.Pole yake kama bado hajaariji wataalam/wabobezi kwenye hiyo taalama kuhusu ushauri....ahakikishe anabakia namafanikio milele hizo picha Tayari hazifutiki pengine
Mzee Kikwete sipingi ana maamuzi ya busara na ushauri wa kutoka moyoni kwa watu. Na kama mtu akikupa ushauri na ukaufata, hakika haupotei njia. Mimi ni mfuasi wa busara zake.
Ila katika maisha yetu, sisi wanyonge/wakulima wa korosho/walimu/wastaafu/wafanya biashara/wapinzani/wasanii/waandishi wa habari/madereva (Nliemsahau mnikumbushe) tunalia na wewe kwa haya maamuzi uliotufanyia 2015.
Mungu anakuona mzee, sijui tulikukosea wapi mzee wetu wewe, mpaka ukatuadhibu na hii adhabu kali sana.
Ulituacha tunakula milo miwili kwa siku, nchi ikiwa na amani. tuliona tujikaze kisabuni, na tukajua ikifika asubuhi/pakipambazuka tutaliona jua na hakika tutafikia malengo yetu, malengo yetu yalikua ni kula milo mitatu tu kwa siku, na wala sio malengo makubwa ya kupanda ndege au treni za umeme.
Ila kumepambazuka, na kweli jua tumeliona, ila kilicho tusibu kimefuta na kuua ndoto zetu zote tulizokua nazo. Badala ya kutafuta mlo wa tatu, sasa tumerudi hatua kadhaa nyuma, na sasa tunakula mlo mmoja, mlo wapili ni kitendawili kisichokua na MAJIBU. Swala la amani nalo ni kitenzi-kishirikishi kwenye ishu ya mlo, tunaamka asubuhi bila kuijua jioni yetu itafika vipi (Kama ni central au mahakamani).[emoji53]
Nikipata nauli kama Platinum, au lifti ya magari makubwa, ntakuja kijijini kukusalimia.
Uislamu wa bagamoyoHuyu Mzee ana maneno ya busara sana na nadhani Uislam wake una siri nzito sana juu ya maisha ya mwanadamu,nitajifunza niuelewe hekima zake.