Dkt. Kikwete Amfungukia Mambo Mazito Diamond Platnumz.

Dkt. Kikwete Amfungukia Mambo Mazito Diamond Platnumz.

Huyu mzee moja ya ahadi zake alizoshindwa kutimiza ni kuileta Real Madrid uwanja wa Taifa. Yaani kaenda mwenyewe tu kupiga picha Bernabéu.
 
Huyu mzee moja ya ahadi zake alizoshindwa kutimiza ni kuileta Real Madrid uwanjawa Taifa. Yaani kaenda mwenyewe tu kupiga picha Bernabéu
Dah umeua kabisa[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Mzee Kikwete sipingi ana maamuzi ya busara na ushauri wa kutoka moyoni kwa watu. Na kama mtu akikupa ushauri na ukaufata, hakika haupotei njia. Mimi ni mfuasi wa busara zake.

Ila katika maisha yetu, sisi wanyonge/wakulima wa korosho/walimu/wastaafu/wafanya biashara/wapinzani/wasanii/waandishi wa habari/madereva (Nliemsahau mnikumbushe) tunalia na wewe kwa haya maamuzi uliotufanyia 2015.

Mungu anakuona mzee, sijui tulikukosea wapi mzee wetu wewe, mpaka ukatuadhibu na hii adhabu kali sana.

Ulituacha tunakula milo miwili kwa siku, nchi ikiwa na amani. tuliona tujikaze kisabuni, na tukajua ikifika asubuhi/pakipambazuka tutaliona jua na hakika tutafikia malengo yetu, malengo yetu yalikua ni kula milo mitatu tu kwa siku, na wala sio malengo makubwa ya kupanda ndege au treni za umeme.

Ila kumepambazuka, na kweli jua tumeliona, ila kilicho tusibu kimefuta na kuua ndoto zetu zote tulizokua nazo. Badala ya kutafuta mlo wa tatu, sasa tumerudi hatua kadhaa nyuma, na sasa tunakula mlo mmoja, mlo wapili ni kitendawili kisichokua na MAJIBU. Swala la amani nalo ni kitenzi-kishirikishi kwenye ishu ya mlo, tunaamka asubuhi bila kuijua jioni yetu itafika vipi (Kama ni central au mahakamani).[emoji53]

Nikipata nauli kama Platinum, au lifti ya magari makubwa, ntakuja kijijini kukusalimia.

Mafisadi ndo walikuwa wanaisha kama malaika....kipindi hiki ni kuishi kama mashetani....Ila sisi wajasiliamali mpaka leo tunakuka Milo mitatu kama kawa na kwa jasho LETU.
 
Back
Top Bottom