Dkt. Kimei na Spika Ndugai, watoto wenu mliwasomesha ufundi simu?


Ili wabaki kuwa wao lazima watengeneze kundi la watu wa chini
 
Una degree ya Mining Engineering basi unarudi kuwa mhadhiri na hata hujapitia kozi ya ualimu. Hivyo 'Pedagogy skills unazitoa wapi?
Niliwahi kuhoji suala kama hili;

 
Ndo maana wanataka mitaala ibadilishwe.
Yaaani mtoto akitoka form 4 au 6 au chuo.
Awe na ujuzi wa ziada.
Hata akikosa ajira ujuzi wake anao utamsaidia.
Sawa kabisa, form four aende ufundi umeme badala ya form five

Ninachotaka kujua, mtoto wa Kimei alienda ufundi umeme ?
 
Vyuo vya ufundi viwe vingi kila mkoa yaani tutatengeneza bonge la taifa kama china kutakuwa na wajuzi wengi na ushindani mkubwa na ugundunduzi wa vitu mbalimbali baada ya miaka 20 tutawapiku wachina sana tu
 
Ndo maana wanataka mitaala ibadilishwe.
Yaaani mtoto akitoka form 4 au 6 au chuo.
Awe na ujuzi wa ziada.
Hata akikosa ajira ujuzi wake anao utamsaidia.
Ujuzi utamsaidia vp wakati hakuna ajira/pesa mitaani? Kama hakuna pesa mtaani hata kama mtoto ana ujuzi wa umeme atafanya wiring nyumba ya nani wakati watu hawajengi? Hata kama wapo wachache wanaojenga hao mafundi umeme au welding wapo wangapi hapo mtaani? Mwenye shibe hawezi kumkumbuka mwenye njaa hata siku moja mkuu.
 
Watoto wenu wakasome ufundi simu ili waweze kupata matonge kwa sababu baba zenu hawana pesa. Watoto wa Kimei na Ndugai wao wataenda kusomea usimamizi wa fedha kwa sababu baba zao wanazo nyingi Sana.
Kwa kiingereza wanasema "it's survival of the fittest" mwenye nacho atazidi kuongezewa
 
Wao wanawapeleka ufundi watoto wao? Au wanataka na vizazi vyao ndiyo wabaki kutawala milele!
 
Naunga mkono hili
 
Sio lazima mkuu.
 
FUNDI HAJAWAHI KUKOSA KAZI.
 
Nijuavyo kuna tofauti kati "teacher" na "instructor"!

Huyo mtu wa mining anakua instructor na sio teacher.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…