Dkt. Luciano Tsere kwa uchache sana

Dkt. Luciano Tsere kwa uchache sana

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
GUMZO LA HARITH GHASSANI: MOHAMED SAID ANAMWELEZA ABDUL SYKES KUTOKEA BURMA INFANTRY 1945, DOCKWORKERS UNION 1949 HADI TAA 1950 NA KUUNDA CHAMA CHA TANU 1954

Baada ya Kipindi Cha Kwanza nilichomzungumza Kleist Sykes fuatilia Kipindi cha Pili namzungumza Abdulwahid Kleist Sykes.

Fuatilia ukurasa huu usikilize historia ya siasa kama zilivyokuwa katika mji wa Dar es Salaam baada ya Vita Vya Pili Vya Dunia.

Yaliyowakuta Waingereza mikononi kwa makuli wa Bandari ya Dar es Salaam mwaka wa 1950 katika maandamano ya kupinga dhulma za serikali ya kikoloni na watalamizi wao hawakuyategemea.

Mambo yalianza baada ya dua na Halal Badr kusomwa Shambani kwa Mohamed Abeid Bonde la Msimbazi watu wakalishana yamini kujikinga na wasaliti.

Makuli wa Bandari ya Dar es Salaam walimwaga katika mitaa ya Dar es Salaam damu zao na za askari Kavirondo Waafrika wenzao waliokuwa wanajiona wao ni sehemu ya mtawala dhalimu.

Yaliyowafika Waingereza kutoka vichwa vya vijana wasomi wa wakati ule waliotokea Makerere tena madaktari wa binadamu, Dr. Vedasto Kyaruzi, Dr. Luciano Tsere, Dr. Wilbard Mwanjisi kuwataja wachache, hayakupata kuwapitia Waingereza hata kwa mbali sana.

In Shaa Allah nitakusomea haya yote kutoka kumbukumbu za wale waliokuwapo wakati ule na kuyaona haya yote kwa macho yao na kuyasikia kwa masikio yao mawili.

Si kweli kuwa uhuru wa Tanganyika ulikuja bila ya kumwaga damu.

Hiki kipindi cha 1945 baada ya Vita Vya Pili Vya Dunia kufikia 1950 kina umuhimu wa pekee katika harakati za kuirekebisha TAA ijizatiti kukabiliana na ukoloni na kuweka msingi imara wa kuunda TANU.

Hapa ndipo unamkuta na Dr. Luciano Tsere na wezake jumla yao madaktari watano pamoja na Dr. Joseph Mutahangarwa, Dr. Vedasto Kyaruzi, Dr. Wilbard Mwanjisi na Dr. Michael Lugazia.

Inakuwaje historia hii na wazalendo hawa leo hawatajwi popote?

Ingekuwaje leo laiti kama Judith Listowel asingewataja katika kitabu chake, "The Making of Tanganyika?"

Picha ya kwanza ni Dr. Luciano Tsere na ya pili ni Abdul Sykes na Ally Sykes wako Burma Vita Vya Pili Vya Dunia.
Screenshot_20210311-080724.jpg
Screenshot_20210308-165737~3.jpg
 
Hata yule mwanamke wa maji maji ungeandika kwa uchache sana
Hata yule mwanamke wa maji maji ungeandika kwa uchache sana
Underwood,
Nimemwandika Dr. Tsere kwa uchache ili kutia hamu wasomaji wangu watambue kuwa ipo historia kubwa ambayo inangojewa kuandikwa.

Nimeandika kwa uchache kwa jili ya kanuni za uandishi.
Dr. Tsere wanae wapo na tumekuwa pamoja toka udogo wetu.

Juzi waliadhimisha kifo cha baba yao kwa makala na nilipoisoma ndipo nami kama kumwadhimisha huyu baba yetu nikaandika machache.
 
Mohammed Said, kumradhi shekh hawa waliomwaga damu walikuwa wanagombea haki zao kama wafanyakazi wa bandari au walikuwa wanagombea uhuru wa Tanganyika yote

Objectives zao zilikuwa ni zipi?
 
Pia shekhe leo utupe ufafanuzi wa chama cha kiislam jina sina uhakika sana AMNUT au kitu kama hicho(All Muslim...), katika kusoma tulikuwa kunaambiwa ni vyazo au sababu zilizochelewesha kwa Tanganyika kujipatia uhuru wake, jamaa walikuwa wanadai waingereza waendelee kutawala hadi pale waislam watakapo ona kuna usawa katika elimu na ni vitu vilichochelewesha sana Tanganyika kujitawala ungekuta tumepata uhuru hata miaka hiyo ya 1945-49
 
Hata yule mwanamke wa maji maji ungeandika kwa uchache sana
Underwood ni ''Maji Maji.''
Yule mwanamama jina ake ni Khadija.

Naona umeghadhibika.
Sijui kipi kibaya nilichosema kukupandisha hamaki.
 
Shakur...
Ningependa kukuuliza swali wewe uliposoma umeelewa nini?
 
Pia shekhe leo utupe ufafanuzi wa chama cha kiislam jina sina uhakika sana AMNUT au kitu kama hicho(All Muslim...), katika kusoma tulikuwa kunaambiwa ni vyazo au sababu zilizochelewesha kwa Tanganyika kujipatia uhuru wake, jamaa walikuwa wanadai waingereza waendelee kutawala hadi pale waislam watakapo ona kuna usawa katika elimu na ni vitu vilichochelewesha sana Tanganyika kujitawala ungekuta tumepata uhuru hata miaka hiyo ya 1945-49
Shakur,
Ningependa kukuuliza maswali na mimi.

Historia uliyosomeshwa uliifunzwa ni watu gani waliasisi African Association?
Ulitajiwa majina yao?

Je, ulifundishwa majina ya Waislam waliounda AMNUT na sababu ya kuundwa chama hicho?

Uhuru wa kupatikana mwaka wa 1945 je walikueleza viongozi wa African Association wa miaka hiyo walikuwa ni akina nani na je walikutajia majina yao?
 
Subirin awaletee historia ya waislam.
Kitali,
Inawezekana historia ya Waislam katika kupigania uhuru wa Tanganyika huipendi.

Hili ni jambo la kawaida.

Kuna watu hawaipendi historia ya Wakikuyu katika kunyanyua silaha chini ya Dedan Kimathi dhidi ya Waingereza kupigania uhuru wa Kenya.

Hili si jambo la kushangaza.
 
Utawadanganya wenye upeo kama wako.
Kitali,
Usighadhibike.
Tufanye mjadala wa kiungwana tujadiliane kwa hoja.

Naona umeghadhibika na maandishi yangu.
Ama kuhusu upeo...

Alhamdulilah si mtu wa kuandika upuuzi.

Ukiwa unataka ithibati ninaweza kukuwekea hapa vitabu nilivyoandika na vyuo nilivyosimama na kuzungumza Afrika, Ulaya na Marekani.
 
Kwa kukusaidia tu wazungu kwa asili wako radh kusikiliza hata ujinga. So kuhutubia marekan ulaya nk haimaanisha uko sahih. Kule hata akienda mganga unapewa jukwaa la kusema
 
Kwa kukusaidia tu wazungu kwa asili wako radh kusikiliza hata ujinga. So kuhutubia marekan ulaya nk haimaanisha uko sahih. Kule hata akienda mganga unapewa jukwaa la kusema
Kitali,
Kuwa Wazungu au binadamu yoyote kuwa radhi kusikiliza upuuzi hapo hujasema kweli.

Hii mosi na pili naalikwa kwa kuwa nimekuja na elimu mpya hawakuwanayo kabla katika moja ya historia za Afrika.

Historia yenyewe ndiyo hii tunayojadili hapa.

Kila unavyozungumza ndivyo ninavyozidi kukufahamu.
 
Dudus,
Utapata shida ukidhani kuwa mimi ni sheikh na wengi hudhani hivyo.

Hapa huzungumzi na sheikh kwani elimu yangu yote ni sekula.

"Amenielewa sheik."
Shukrani Mkuu. Ila kwa mujibu wa Wikipedia (Sheikh), hilo neno lina maana kadhaa; The term can be literally translated to "Elder". Mimi nilirejea hiyo.
 
Back
Top Bottom