Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
GUMZO LA HARITH GHASSANI: MOHAMED SAID ANAMWELEZA ABDUL SYKES KUTOKEA BURMA INFANTRY 1945, DOCKWORKERS UNION 1949 HADI TAA 1950 NA KUUNDA CHAMA CHA TANU 1954
Baada ya Kipindi Cha Kwanza nilichomzungumza Kleist Sykes fuatilia Kipindi cha Pili namzungumza Abdulwahid Kleist Sykes.
Fuatilia ukurasa huu usikilize historia ya siasa kama zilivyokuwa katika mji wa Dar es Salaam baada ya Vita Vya Pili Vya Dunia.
Yaliyowakuta Waingereza mikononi kwa makuli wa Bandari ya Dar es Salaam mwaka wa 1950 katika maandamano ya kupinga dhulma za serikali ya kikoloni na watalamizi wao hawakuyategemea.
Mambo yalianza baada ya dua na Halal Badr kusomwa Shambani kwa Mohamed Abeid Bonde la Msimbazi watu wakalishana yamini kujikinga na wasaliti.
Makuli wa Bandari ya Dar es Salaam walimwaga katika mitaa ya Dar es Salaam damu zao na za askari Kavirondo Waafrika wenzao waliokuwa wanajiona wao ni sehemu ya mtawala dhalimu.
Yaliyowafika Waingereza kutoka vichwa vya vijana wasomi wa wakati ule waliotokea Makerere tena madaktari wa binadamu, Dr. Vedasto Kyaruzi, Dr. Luciano Tsere, Dr. Wilbard Mwanjisi kuwataja wachache, hayakupata kuwapitia Waingereza hata kwa mbali sana.
In Shaa Allah nitakusomea haya yote kutoka kumbukumbu za wale waliokuwapo wakati ule na kuyaona haya yote kwa macho yao na kuyasikia kwa masikio yao mawili.
Si kweli kuwa uhuru wa Tanganyika ulikuja bila ya kumwaga damu.
Hiki kipindi cha 1945 baada ya Vita Vya Pili Vya Dunia kufikia 1950 kina umuhimu wa pekee katika harakati za kuirekebisha TAA ijizatiti kukabiliana na ukoloni na kuweka msingi imara wa kuunda TANU.
Hapa ndipo unamkuta na Dr. Luciano Tsere na wezake jumla yao madaktari watano pamoja na Dr. Joseph Mutahangarwa, Dr. Vedasto Kyaruzi, Dr. Wilbard Mwanjisi na Dr. Michael Lugazia.
Inakuwaje historia hii na wazalendo hawa leo hawatajwi popote?
Ingekuwaje leo laiti kama Judith Listowel asingewataja katika kitabu chake, "The Making of Tanganyika?"
Picha ya kwanza ni Dr. Luciano Tsere na ya pili ni Abdul Sykes na Ally Sykes wako Burma Vita Vya Pili Vya Dunia.