Dkt. Luciano Tsere kwa uchache sana

Dkt. Luciano Tsere kwa uchache sana

Pia shekhe leo utupe ufafanuzi wa chama cha kiislam jina sina uhakika sana AMNUT au kitu kama hicho(All Muslim...), katika kusoma tulikuwa kunaambiwa ni vyazo au sababu zilizochelewesha kwa Tanganyika kujipatia uhuru wake, jamaa walikuwa wanadai waingereza waendelee kutawala hadi pale waislam watakapo ona kuna usawa katika elimu na ni vitu vilichochelewesha sana Tanganyika kujitawala ungekuta tumepata uhuru hata miaka hiyo ya 1945-49
AMNUT ikaundwa 1959 ije kuzuiya uhuru 1945 ama 1946? Hiyo miaka hata TANU haijazaliwa .cha!
 
Shukrani Mkuu. Ila kwa mujibu wa Wikipedia (Sheikh), hilo neno lina maana kadhaa; The term can be literally translated to "Elder". Mimi nilirejea hiyo.
Dudus,
Tumia baba kama unapenda kuniwekea staha kwani "Sheikh," kwa hapa litapelekea maana siyo.
 
AMNUT ikaundwa 1959 ije kuzuiya uhuru 1945 ama 1946? Hiyo miaka hata TANU haijazaliwa .cha!
Baliba...
AMNUT iliasisiwa mwaka wa 1958 Rais akiwa Abdallah Mohamed na Katibu Ramadhani Mashado Plantan.

Kisa cha AMNUT nimekieleza kwa kirefu katika kitabu cha Abdul Sykes.

Hakikuwa chama cha Waislam kwa maana halisi kwani kama kuna chama kilikuwa cha Waislam basi ni TANU.

AMNUT kingekuwa chama cha Waislam kisingekosa wanachama hadi kupelekea kufa.
 
AMNUT ikaundwa 1959 ije kuzuiya uhuru 1945 ama 1946? Hiyo miaka hata TANU haijazaliwa .cha!
Inawezekana hiyo 1959 ndio walikisajili officially kama chama cha siasa ila mwamko wao ulianza toka Mwalimu alivyounda TANU na kuchukua kadi yake nambari 1.
 
Inawezekana hiyo 1959 ndio walikisajili officially kama chama cha siasa ila mwamko wao ulianza toka Mwalimu alivyounda TANU na kuchukua kadi yake nambari 1.
Shakur,
Mwalimu hajaunda TANU.

Kadi No. 1 aliandikiwa na Ally Sykes kadi ya Territorial President.

Kadi ya Mwalimu ukiitazama utakuta ina saini ya Ally Sykes.

Kadi No. 2 ya Ally Sykes.
Kadi No. 3 ya Abdulwahid Sykes.

Umeanza vibaya kuiunganisha AMNUT na Nyerere kuunda TANU.

Hiki kisa kinatoka mbali tokea mwaka wa 1929 Kleist Sykes baba yao Abdul na Ally alipokuwa katibu muasisi wa African Association.

Katika hali hii Mwalimu atawezaje kuunda TANU?
Ataingia kwa mlango upi aunde TANU?
 
Back
Top Bottom