Mtu mwenye tabia ya aina fulani hawezi kubadilika sanasana atajivika ngozi ya Kondoo tu ili apate kura kisha anabaki kwenye uhalisia wake.
Ni jukumu la usalama wa Taifa kutusaidia wanataka nchi iwe na vipaumbele vipi. Je wanakubaliana na haya makandokando yaliyopo?. (No uhuru, No mshikamano wa Taifa, umimi, ukata mkali, ukabila, kujimwambafai, misifa camp, visasi - ukichagua mpinzani = No maendeleo kisha anafanya kweli)
Au watu wa Kitengo watakubali kutupa chata nyingine mpya inayofanana na Magufuli ila ina vitu vingine vizuri vya ziada ili kuirejesha nchi kwenye amani na furaha ya kweli toka moyoni kwa kutuachia mtu toka kabila dogo mwenye upendo na kila mtu na asiye na makandokando.
Ukiangalia ilani ya uchaguzi ya CCM, Utagundua kuwa huyu jamaa hana mpango wa kubadilika, mwendo ni uleule wa muendelezo wa miaka mitano iliyopita.