Deogratias Mutungi
Senior Member
- Oct 1, 2019
- 140
- 181
Nawasalimu wana JF.
Kwa ufupi nagusia uvumi na maneno yanayosambazwa mitandaoni kuwa Mgombea wa CCM Dkt Magufuli amekataliwa Mkoani Kagera na wala hakubaliki hasa katika kipindi hiki cha uchaguzi mkuu, Nawajulisha kuwa utafiti uliopo unaonyesha wazi kuwa Mgombea wa CCM anakubalika kwa asilimia kubwa ambazo zitampa ushindi wa kishindo ndani ya Mkoa huo na viunga vyake, Magufuli hana sababu za kutokubalika, Kama ni Maendeleo ya watu na vitu yamefika kwa wanakagera, CCM na serikali ya awamu ya tano kamwe hawajawai kuwa bagua watu wa Kagera, nashauri tuache propaganda za kutumia utani wa Dkt Magufuli kufitinisha watu/Watanzania, tujenge hoja hasi za kunadi sera kwa msingi wa maendeleo ya taifa letu na si propaganda mgando, hazifai hata kidogo na ni kikwazo cha maendeleo.
Aidha hoja ya kutumia dhana ya tetemeko kujenga hoja za upotoshaji nashauri tuziweke pembeni na badala yake, tugeukie kumulika maendeleo ya sasa kwa mantiki ya miundo mbinu na vitu vingine baada ya tetemeko vimekaaje tuache chuki, ghiliba, upotoshaji na lawama kwa Magufuli badala yake tujikite kupima mazuri ya miaka mitano ya utawala wake na tuone kama anafaa kupewa nafasi ya uongozi tena au hafai, bila shaka wote tunatambua mazuri ya JPM kwa kipindi cha miaka mitano, hivyo basi myonge myongeni lakini haki yake mpeni. Kwa kuhitimisha andiko hili fupi ni kuwa Wana Kagera wana imani na Dkt Magufuli na wapo tayari kumtuma tena kwa kipindi cha miaka mingine mitano kwa sababu sifa, uwezo, utashi, hekima na ubunifu vyote anavyo ambavyo ndio nguzo ya uongozi bora na imara.