Uchaguzi 2020 Dkt. Magufuli anatakiwa ajue kuwa Kampeni ni kujishusha, sio kufokea na kuwatisha wapiga kura

Uchaguzi 2020 Dkt. Magufuli anatakiwa ajue kuwa Kampeni ni kujishusha, sio kufokea na kuwatisha wapiga kura

Quinine

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2010
Posts
22,227
Reaction score
49,628
Ninachojua mimi kura ni siri ya mpiga kura, kura ni haki ya mpiga kura, kura sio haki ya mgombea kuwa ataidai kwa lazima, kuwa asipopigiwa atawaadhibu wapiga kura.

Mgombea wa CCM anadhani kupigiwa kura ni haki yake analazimisha, anawafokea wapiga kura na kuwatisha.

Naomba Magufuli ajifunze kwa watangulizi wake walivyo kuwa wanafanya kampeni, Mwinyi hakuwa hivyo, Mkapa pamoja na ubabe wake lkn alijishusha, Kikwete ndiyo kabisa hadi chini alikaa, si kwamba hawakuwa na mamlaka yote kama yake lkn walikuwa ‘humble’, walikuwa karibu na wapiga kura wao.

The meaning of campaign is to maximize the little you have, even a single vote counts.

Unapomfokea mpiga kura unapomtisha kuwa hutamletea maendeleo, maana yake ni nini, hata kama alikuwa amepanga kukupigia kura anaweza kusita, atajiuliza kama hata kabla ya kumpigia ananitisha namna hii, je nikishampigia na akiwa na uhakika wa kura yangu si ataniumiza zaidi.

Magufuli ajue kura ni siri, akumbuke wapiga kura ni wajumbe sio wa kuwaamini sana kwa 100%, leo wanaweza kukwambia tuko pamoja lakini siku ya trh 28 Oktoba wakakushangaza.
 
Lazima uelezwe kwa lugha nyeupe.kwamba ukijichanganya utakula ulioopeleka mboga.

Wale walizomea Bukoba watampa kura rais wao wanayempenda, akipita wameula, asipopita wamelamba joker, kama kubeti yaani.
 
Lazima uelezwe kwa lugha nyeupe.kwamba ukijichanganya utakula ulioopeleka mboga.

wale walizomea bukoba watampa kura rais wao wanayempenda,akipita wameula, asipopita wamelamba joker,kama kubeti yaani.
Halafu unaendelea kukusanya kodi kutoka kwao?Fanyeni ujinga mtukaribishie kama ya sudani! Upendeleo katika maendeleo ndio umesababisha uasi mpaka leo nchi imegawanywa vipande viwili!
 
Mnaotishika na ufokeaji ni CHADEMA na magenge yenu, tulieni sindano iwaingie.

Watu wema hawana mashaka na hiyo sauti.

Sauti ya Simba haimtishi mwanae bali vi wanyama dokozi ndo vina anza kukimbia.
 
Mtu aliekuwa akimtaja Mungu kila dakika na katika kila muhadhara leo hii kashindwa kuiga hata moja juu ya milioni ya matendo ya mfalme Selemani? Vitisho na ubaguzi wazi wazi. Ama Kweli si kila asemae Bwana, Bwana ataurithi ufalme wa mbinguni.
 
Halafu unaendelea kukusanya kodi kutoka kwao?Fanyeni ujinga mtukaribishie kama ya sudani. Upendeleo katika maendeleo ndio umesababisha uasi mpaka leo nchi imegawanywa vipande viwili!

Sudan imechafuka sababu ya ulafi wa madaraka. Kama unaona wanapa raha kuliko uliyonayo sasa hivi utapelekwa sudan wewe peke yako kama wale wa uamsho nk.

Msitake kuivuruga nchi kwa tamaa zenu za fisi.
 
Mnaotishika na ufokeaji ni chadema na magenge yenu, tulieni sindano iwaingie,
Watu wema hawana mashaka na hiyo sauti.

Sauti ya Simba haimtishi mwanae bali vi wanyama dokozi ndo vina anza kukimbia.

Mtu anakwambia patachimbika, halafu haoni tatizo alilonalo[emoji28][emoji28].
 
Back
Top Bottom